Na Alex Mapunda,Iringa
Timu ya Lipuli
toka mkoani Iringa imewadhiirishia wadau wa soka mkoa Iringa kuwa imepania
kupanda ligi kuu baada ya kuwakung’uta watani wao wajadi Kurugenzi toka Mafinga
bao 1-0 katika mtanange wa ligi daraja la kwanza uliofanyika kwenye uwanja wa
Samora,juzi.
Katika mchezo
huo ambao ulikuwa mkali dakika zote 90,timu hizo zilianza kushambuliana zamu kwa
zamu toka dakika ya kwanza lakini bahati ilikuwa kwa upande wa Lipuli baada ya Jafari Hathumani Gonga kukwamisha
mpira kimiani dakika ya 45 kwa ufundi mkubwa kwa faulo kufatia George mpole kumfanyia
madhambi mchezaji wa Lipuli nje ya 18 ambaye alizawadiwa kadi nyekundu.
Kurungezi walikuja
juu kwa kufanya mashambulizi langoni mwa Lipuli lakini walinzi wa Lipuli walikuwa
Imara huku wakiakikisha ngome yao
haiteteleki ambapo hadi dakika 90 zilipokamirika Lipuli waliibuka kededea kwa
ushindi wa bao 1-0.
Kivutio
kikubwa katika mchezo huo walikuwa ni mashabiki wa timu ya Lipuli wakiongozwa
na Salum Kisako ambao wanauchu wa kuona timu yao ikipanda ligi kuu ambapo
walishangilia kwa muda wote huku wakisema hawawezi kufungwa na wakata magogo
toka Mafinga.
Baada ya
kumalizika mchezo huo Kaimu mwenyekiti wa Lipuli Renatus Karinga alitoa maneno makali ya kisoka kuwa Lipuli
ikifungwa na Kurugenzi ataachana na masuala yanayohusu kandanda,huku akiwa
amejawa na furaha kubwa ya ushindi.
Lipuli sasa
imefikisha pointi 20 ponti 1,nyuma ya Friend Rengers ambao nao wamemaliza mechi
zao za mzunguko wa kwanza.
Chapisha Maoni