WEKUNDU wa msimbazi Simba wameendeleza wimbi la kutoa sare mara baada ya hii leo kutoshana nguvu dhidi ya mtibwa sugar toka Tuliani Morogoro katika mtanange wa ligi kuu ya vocom Tanzania bara uliopigwa katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Simba walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 35 kupitia kwa mganda Joseph Owino bao ambalo lilidumu hadi wakati wa mapumziko.
Kipindi cha pili watoto wa Tobias Kifaru walikuja juu ambapo mnamo dakika ya 58 Musa Hasan Mgosi ndiye aliyewaua simba na ubao ukasomeka bao moja kwa moja.
Mtibwa
Sugar; Said Mohammed, Hassan Ramadhani, David Luhende, Andrew Vincent, Salim
Mbonde, Shaaban Nditi, Mussa Ngosi, Mohamed Ibrahim, Ame Ally, Mussa Nampaka na
Ally Shomary.
Simba SC; Peter Manyika, William Lucian ‘Gallas’, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Joseph Owino, Jonas Mkude, Ramadhani Singano ‘Messi’, Awadh Juma, Elias Maguri/Amisi Tambwe dk76, Said Ndemla na Emmanuel Okwi/Uhuru Suleiman dk75.
Mechi za leo14/11/01
KAGERASUGAR | 1 | : | 0 | YANGASC |
COASTALUNION | 1 | : | 0 | RUVUSHOOTING |
JKTRUVU | 1 | : | 1 | PolisiMorogoro |
NDANDAFC | 1 | : | 0 | AZAMFC |
STANDUNITED | 1 | : | 1 | T.PRISONS |
MTIBWASUGAR | 1 | : | 1 | SIMBASC |
Chapisha Maoni