Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




IRINGA
Na alex mapunda,Iringa

Timu ya Lipuli mkoani Iringa Imevutwa shati tena katika uwanja wake wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na polisi ya Jijini Dar es salam ,katika mchezo wa ligi daraja la kwanza uliofanyika katika uwanja wa samora mkoani Iringa.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa na mashambulizi mengi, Lipuli ilikuwa ya kwanza kupata ushindi dakika ya 12 ya mchezo kupitia kwa nahodha Ramadhani kudunda, bao ambalo lilidumu adi dakika 45 kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili polisi ya Dar es salam walitumia vema madhaifu ya safu ya ushambuliaji ya lipuli pamoja na kupwaya kwa sehemu ya kiungo ya lipuli na kusawazisha bao hilo ambapo adi dakika 90 za mchezo Lipuli walitoka uwanjani vichwa chini baada ya kuendeleza wimbi la sare.

Katika mchezo uliopita timu ya Lipuli ilitoka sare na Tessema Fc katika uwanja wa nyumbani ambapo  Lipuli  inatakiwa kucheza kwa kujituma zaidi ili kuhakikisha inapanda daraja mara baada ya kucheza madaraja ya chini kwa muda mrefu bila mafanikio.

Kwa upande mwingine timu ya Kurugenzi ya mafinga nayo imefungwa bao 2-1 dhidi ya African Sports  katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa mkwakwani Mkoani Tanga.


Chapisha Maoni