Michuano ya Ligi Daraja la Pili (SDL) msimu huu iliyokuwa
ianze kutimua vumbi Novemba 22 mwaka huu kwa mechi kumi katika viwanja
vitano tofauti imesogezwa mbele hadi Desemba 6 mwaka huu.
Mechi hizo zimesogezwa ili kutoa fursa ya kukamilisha maandalizi mbalimbali ya ligi hiyo inayoshirikisha timu 24 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.
Mikoa yenye timu katika ligi hiyo ni Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Katavi, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Njombe, Pwani, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Singida na Tabora.

Chapisha Maoni