Aliyekuwa kocha wa Yanga, Mbrazil
Marcio Maximo ameondoka jana kurudi nyumbani kwao Brazil na kuitakia klabu yake
ya zamani kila la kheri.
Maximo na Mbrazil mwenzake, Leonardo
Neiva wametupiwa virago na mabingwa hao wa zamani hivi karibuni kwa kile
kinachoelezwa kufanya vibaya kwa timu hiyo inayojiandaa na michuano ya vilabu
ya shirikisho la soka Afrika hapo mwakani.‘Nawashukuru viongozi wa Yanga na
mashabiki kwa muda tuliokaa pamoja”.” Yanga ni klabu kubwa yenye malengo”.
“Nilikuwa na malengo ya kuiongoza
Yanga kitaalamu zaidi, lakini inaonekana fikra zangu hazikueleweka na kuungwa
mkono”.
“Tayari kuna vilabu kadhaa
vimeonesha nia ya kuniajiri lakini nitahitaji muda kidogo kufikiria”, alisema
kocha huyo aliyewahi kuifundisha timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars).
Maximo ameitumikia Yanga kwa miezi
mitatu na kucheza mechi tisa. Katika hizo, amefungwa mechi mbili, moja hivi
karibuni Yanga walipocheza na mahasimu wao Simba iliyochini ya kocha Mzambia
Patrick Phiri na kufungwa 2-0 katika mechi isiyo ya ligi.
Chapisha Maoni