Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




KUKOSEKANA kwa Uzio na Usalama hafifu katika uwanja wa michezo wa Samora mkoani  Iringa imeelezwa kuwa ndio chanzo cha timu ya soka ya  Friends Rangers kupoteza mchezo wake dhidi ya Lipuli uliofanyika uwanjani hapo  hivi karibuni kwa kufungwa bao 1-0.
Akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya mchezo huo kumalizika kocha wa Friends Rangers Ally Mzozo alisema kuwa uwanja wa samora sio salama kutokana na kutokuwepo uzio hali ambayo inapelekea mashibiki kushangilia hadi uwanjani bao likiingia.
“Sheria za TFF ziko wazi uwanja ambao hauna uzio usitumike,ni hatari kwa wachezaji kama mashabiki wanashangilia watakavyo uwanjani,Tff na viongozi wa mkoa walitanzame suala hilo”alisema mzozo.
Vile vile mzozo aliongeza kuwa hali ya usalama katika uwanja wa Samora sio zuri ambapo viongozi kwa wanatakiwa kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha wanakuwepo polisi wa kutosha uwanjani hapo wakati wa michezo mbali mbali.
Uwanja wa samora mkoani Iringa unaitaji matengenezo makubwa ambapo moja ya vitu ambavyo inatakiwa virekebishwe ni Sehemu ya kuchezea,uzio,pamoja na vyumba vya kubadilishia nguo.


Chapisha Maoni