Orodha hifuatayo inaonesha wachezaji
waliosajiliwa dirisha dogo, waliotemwa na kutolewa kwa mkopo na timu mbalimbali
zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL);
AZAM FC; walioingia ni Wawa, Majwega
na Amri Kiemba. Waliotoka ni Ismail Diara raia wa Mali (katemwa) na Mhaiti Lionel
Saint-Preux (katemwa).
YANGA; walioingia ni Sherman, Amissi
Tambwe, Danny Mrwanda, Athuman Majogo (Friends Rangers) na Emerson (amesajiliwa
na kutemwa). Walioondoka ni Hamis Kiiza (katemwa), Omega Seme (mkopo Ndanda
FC), Hamis Thabit (mkopo Stand United), Geilson Santos Santana ‘Jaja’
(ametemwa) na Said Bahanunzi (mkopo Polisi Morogoro).
SIMBA; walioingia ni Sserunkuma,
Simon Sserunkuma, Murshid na Hassan Kessy (Mtibwa Sugar). Walioondoka ni Kiemba
(Azam), Miraj Adam (mkopo Mtibwa Sugar), Haroun Chanongo (mkopo Stand United),
Joram Mgeveke (mkopo Mwadui FC) na Uhuru Seleman (Mwadui FC – Uhuru kavunja
mkataba Simba).
COASTAL UNION; walioingia ni Humud
na Geofrey Wambura (huru), Bakari Thabit (Friends Rangers). Walioondoka ni
Razak Khalfan (mkopo Mwadui FC), Peter Heri (katemwa).
STAND UNITED; walioingia ni Hamis Thabit (Yanga), Chanongo (Simba), Nduwimana
(Burundi), Shaban Kondo, Chinedu, Hamis Shengo na Misheto (Ujerumani).
Walioondoka ni Nelson Kimath na Omar Mtaki (wote Geita FC), Hussein Chepe na
Lucas Charles (wote Polisi Tabora), Robert Magadula na Patrick Mrope (wamevunja
mikataba).
MTIBWA SUGAR; walioingia ni Henry
Joseph (huru) na Miraj (mkopo Simba) na Ibrahim Jeba (huru). Walioondoka ni
Hassan Kessy (Simba).
Ndanda FC; walioingia ni Omega
(Yanga), Kigi Makasi (huru). Stamili Mbonde (Villa Squad), Raymond Zabron
(Villa Squad), Issa Said (huru), Mohamed Masou (huru) na Zuberi Ubwa (huru).
Walioondoka ni Amri Msumi (mkopo Kurugenzi Iringa) na Hamis Saleh (huru).
KAGERA SUGAR; hakuna aliyeingia wala
kutoka.
MBEYA CITY; Kipa Kalyesubula
Hannington (huru), Juma Issa ‘Nyoso’ (huru), Idrisa Rashid, Fredy Cosmas,
Soneka Peter (U20) na Selemani Hassan (U20). Walioondoka ni Anthony matogolo
(mkopo Panone FC), Saad Kipanga (mkopo Polisi Tabora), Ramadhani Abdu (mkopo
Majimaji FC), Medson Mwakatundu – U20 (mkopo Rhino Rangers), Ramadhani Kapela –
U20 (mkopo Coca Cola Mbeya), Majid Shabani – U20 (mkopo Coca-Cola Mbeya),
Abdalah Said – U20 (mkopo Coca-Cola Mbeya) na Waziri Ramadhani – U20 (mkopo
Burkinafaso FC).
TANZANIA PRISONS; hakuna aliyeingia
wala kutoka.
POLISI MOROGORO; walioingia ni Said
Bahanunzi (Yanga), Zahoro Pazi (huru), Meshack Abel (KCB, Kenya) na Iman
Mapunda (huru). Walioondoka ni Danny Mrwanda (Simba), Makungu Siame (mkopo
Malindi, Unguja), Emilian Mgeta (mkopo Villa Squad) na Mosses Mtitu (Majimaji
FC).
RUVU SHOOTING; walioingia ni Mwita
Kimaronge (Toto Africans), Betram Mwombeki (huru), Yahya Tumbo (Mtendeni FC,
Zanzibar) na Ally Yusuph (Ruvu Shooting B).
JKT MGAMBO; hakuna aliyeingia wala
kutoka.
JKT RUVU: hakuna wapya na hawajauza
wala kuoa mchezaji kwa mkopo.
Chapisha Maoni