Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.






MICHUANO ya  Afcon, inaanza kutimua vumbi leo  (januari 17) kuanzia majira ya saa 1:00 usiku nchini Gabon kwa mechi mbili za kundi A kupigwa.
Mechi ya ufunguzi itawakutanisha Guinea ya Ikweta dhidi ya Congo katika kipute cha cha kwanza cha kundi A uwanja wa Estadio de Bata.
Mechi ya pili ya kundi hilo itakuwakutanisha Burkina Faso na wenyeji Gabon katika uwanja huo huo.
Kesho januari 18, Zambia wataoneshana kazi na Congo DR  katika mechi ya kundi B itakayopigwa uwanja wa Nuevo Estadio de Ebebiyín, baadaye Tunia watachuana na Visiwa vya Cape Verde.
Jumatatu januari 19, timu ya taifa ya Ghana, Black Stars itashuka dimbani kuchuana na Simba Wateranga, Senegal katika mechi ya kwanza ya kundi C itayopigwa uwanja wa Estadio de Mongomo.
Mechi ya pili ya kundi C itawakutanisha Aligeria dhidi ya Africa kusini katika uwanja huo huo.


Chapisha Maoni