Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




 Steven Gerrard ameweka wazi kinachomwondoa Leverpool ikiwemo,kwenda kwa wakati hali ambao imesababisha baadhi ya mechi kutokea nje.
Akizungumza katika mahojiano na runinga ya klabu hiyo, Gerrard amesema alipoitwa na kocha Brendan Rodgers na kuambiwa wakati uliwadia wa kufuatilia kwa karibu uchezaji wake.

Baadaye alianza kutokea benchi, jambo ambalo aliamini ilikuwa ni sawa na kauli ya mafumbo, kwamba nafasi yake ni finyu.
“Naelewa, ila ulikuwa ni uamuzi mgumu sana. Nimekuwa Liverpool muda mwingi. Baada ya mazungumzo yetu nikajua kuna jambo hivyo ni lazima nilifanyie kazi,” alisema Gerrard.
“Bado nina miezi sita, nahitaji kujituma na kuisaidia klabu. Nikiondoka, bado siku moja ningependa tena kurejea.

“Kama nitakuwa kocha au vinginevyo, ningependa kuja kuendeleza mchango wangu kwa Liverpool,” alisema Gerrard aliyejiunga na Liverpool akiwa na miaka nane.



Chapisha Maoni