LEO ndio leo ambapo FIFA wanatarajia kumtangaza mchezaji Bora duniani 2014 Ballon D’or katika ukumbi wa Kongresshuas zurich Uswis.
Wanaogombania Tuzo hiyo ni Cristiano Ronaldo wa Klabu ya Real Madrid, Manuel Neuer wa Bayern Munich na Lionel Messi wa Barcelona.
Ronaldo ndie alitwaa Tuzo hiyo Mwaka Jana, ikiwa ni mara yake ya pili, wakati Messi ameitwaa mara 4 mfululizo kabla ya hapo.
Neuer hajawahi kuitwaa Tuzo hii na ameingia tu kwenye kinyang’anyiro hiki baada ya kuisaidia Klabu yake Bayern Munich kutwaa Ubingwa wa Bundesliga na pia Nchi yake Germany kutwaa Kombe la Dunia huko Brazil Mwaka Jana.
Mshindi wa FIFA Ballon d’Or hupatikana toka Kura za Makocha na Manahodha wa Timu za Taifa za Nchi 209 Wanachama wa FIFA pamoja na Wawakilishi maalum toka Wanahabari kutoka Jarida la France Footbal.
Sambamba na FIFA Ballon d'Or pia atatangazwa Kocha Bora Duniani kwa Mwaka 2014 na Wagombea wake ni Kocha wa Mabingwa wa Ulaya Real Madrid, Carlo Ancelotti, Kocha wa Mabingwa wa Dunia Germany, Joachim Low na Kocha wa Mabingwa wa Spain Atletico Madrid, Diego Simeone.
Pia hiyo Jumatatu atatangazwa Mshindi wa FIFA Puskás Award ambayo ni Tuzo ya Goli Bora la Mwaka lililofungwa kati ya 3 Oktoba 2013 and 26 Septemba 2014 na hili huchaguliwa kutokana na Kura za Umma kupitia Mtandao wa FIFA na France Football.
Wagombea wa Goli Bora ni Mwanadada Stephanie Roche aliefungia Klabu yake Peamount United, James Rodriguez aliefungia Colombia dhidi ya Uruguay na Robin van Persie alipofunga Bao la Kichwa cha kuruka wakati Nchi yake Holland inacheza na Spain.
Pia kwenye Hafla hiyo utakuwepo uteuzi wa Kikosi Bora Duniani, FIFA FIFpro World XI, ambacho kitatumia Mfumo wa 4-3-3 yaani yupo Kipa, Mabeki 4, Viungo 3 na Mafowadi 3.
Kwa Kinamama, Mchezaji Bora Duniani atatokana na Wagombea Watatu ambao ni Nadine Kessler, Marta na Abby Wambach ambao pia watakuwa na Kocha wao Bora wa Mwaka huku Wagombe wao wakiwa . Ralf Kellermann, Maren Meinert na Norio Sasaki.
Na kama ilivyo desturi kwa Miaka ya hivi karibuni, Rais wa FIFA hutoa Tuzo maalum, FIFA Presidential Award, kwa Mtu anaetoa mchango bora katika Soka.
Vile vile ipo Tuzo ya Fair Play, Uchezaji wa Haki, na Mshindi wake huteuliwa na Kamati ya FIFA ya Uchezaji wa Haki na Wajbu wa Jamii.
Winners
Until 2010, the best player in the world won the Ballon d'Or or the FIFA World Player of the Year award | |||||
Year | 1st | 2nd | 3rd | ||
---|---|---|---|---|---|
2010 | Lionel Messi (Barcelona) | Andrés Iniesta (Barcelona) | Xavi (Barcelona) | ||
2011 | Lionel Messi (Barcelona) | Cristiano Ronaldo (Real Madrid) | Xavi (Barcelona) | ||
2012 | Lionel Messi (Barcelona) | Cristiano Ronaldo (Real Madrid) | Andrés Iniesta (Barcelona) | ||
2013 | Cristiano Ronaldo (Real Madrid) | Lionel Messi (Barcelona) | Franck Ribéry (Bayern Munich) |
Chapisha Maoni