Tukiendelea kukuletea taarifa za
michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, yanayoendelea nchini Equatorial
Guinea, jana usiku Congo iliweza kupata pointi tatu muhimu baada ya
kuibwaga Gabon bao 1-0.
Katika mzunguko wa kwanza Congo ilitoka
sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji Equatorial Guinea, huku Gabon
ikiicharaza Burkina Faso mabao 2-0. Congo imepata ushindi wake wa kwanza
katika michauno ya Kombe la Mataifa ya Afrika tangu fainali za mwaka
1974. Bao la Congo lilipatikana katika dakika ya 48 likifungwa na
Oniangué. Congo ndiyo inayoongoza kundi A kwa kuwa na pointi 4
ikifuatiwa na Gabon yenye pointi 3, wenyeji Equatorial Guinea wakiwa
katika nafasi ya tatu na pointi mbili. Mwisho ni Burkina Faso yenye
pointi 1, baada ya jana kutoka sare ya kutofungana na wenyeji Equatorial
Guinea katika mzunguko wa pili wa kundi A. Katika mchezo wa mapema wa
kundi hili, Equatorial Guinea na Burkina Faso zimeshindwa kutambiana
baada ya kukamilisha dakika 90 za mchezo zikiwa hazijafungana na hivyo
kugawana pointi moja moja.Sare yoyote na Burkina Faso Jumapili katika mzunguko wa tatu wa kundi A utaiwezesha Congo kufuzu kucheza hatua ya robo fainali. Kadhalika atakayeshinda kati ya Gabon na Equatorial Guinea katika mchezo wa Jumapili huko Bata, pia atafuzukuingia katika hatua ya timu nane yaani robo fainali.
Leo usiku ni mtifuano wa timu za kundi B, ambapo mchezo wa kwanza utazikutanisha Zambia na Tunisia na baadaye Cape Verde na DR Congo. Timu za kundi hili zote zina pointi moja moja.
Nayo timu ya Tanzania, Taifa Stars leo inakabiliana na majirani zao Rwanda katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaochezwa katika mji wa Mwanza magharibi mwa Tanzania. Mwandishi wetu Shadrack Mwansasu ameandaa taarifa ifuatayo:
Na nchini Hispania Barcelona imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Atletico Madrid katika michuano ya Copa del Rey hatua ya robo fainali. Bao la Barcelona limefungwa na Lionel Messi katika dakika ya 85. Timu hizi zitarudiana katika uwanja wa Atletico Madrid, Jumatano ya tarehe 28 mwezi huu.
AFCON 2015
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Januari 17
Equatorial Guinea 1 Congo 1
Burkina Faso 0 Gabon 2
Jumapili Januari 18
Zambia 1 Congo DR 1
Tunisia 1 Cape Verde Islands 1
Jumatatu Januari 19
Ghana 1 Senegal 2
Algeria 3 South Africa 1
Jumanne Januari 20
Côte d'Ivoire 1 Guinea 1
Mali 1 Cameroon 1
Jumatano Januari 21
KUNDI A
Equatorial Guinea 0 Burkina Faso 0
Gabon 0 Congo 1
Alhamisi Januari 22
KUNDI B
1900 Zambia v Tunisia [Nuevo Estadio de Ebebiyín]
2200 Cape Verde Islands v Congo DR [Nuevo Estadio de Ebebiyín]
Ijumaa Januari 23
KUNDI C
1900 Ghana v Algeria [Estadio de Mongomo]
2200 South Africa v Senegal [Estadio de Mongomo]
Jumamosi Januari 24
KUNDI D
1900 Côte d'Ivoire v Mali [Nuevo Estadio de Malabo]
2200 Cameroon v Guinea [Nuevo Estadio de Malabo]
Jumapili Januari 25
KUNDI A
2100 Gabon v Equatorial Guinea [Estadio de Bata]
2100 Congo v Burkina Faso [Nuevo Estadio de Ebebiyín]
Jumatatu Januari 26
KUNDI B
2100 Congo DR v Tunisia [Estadio de Bata]
2100 Cape Verde Islands v Zambia [Nuevo Estadio de Ebebiyín]
Jumanne Januari 27
KUNDI C
2100 South Africa v Ghana [Estadio de Mongomo]
2100 Senegal v Algeria [Nuevo Estadio de Malabo]
Jumatano Januari 28
KUNDI D
2100 Cameroon v Côte d'Ivoire [Nuevo Estadio de Malabo]
2100 Guinea v Mali [Estadio de Mongomo]
ROBO FAINALI
Jumamosi Januari 31
1900 Mshindi Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi B [Estadio de Bata]=RF1
2200 Mshindi Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A [Nuevo Estadio de Ebebiyín]=RF2
Jumapili Februari 1
1900 Mshindi Kundi C v Mshindi wa Pili Kundi D [Estadio de Mongomo]=RF3
2200 Mshindi Kundi D v Mshindi wa Pili Kundi C [Nuevo Estadio de Malabo]=RF4
NUSU FAINALI
Jumatano Februari 4
2200 RF 1 v RF4 [Estadio de Bata]=NF1
Alhamisi Februari 5
2200 RF2 v RF3 [Nuevo Estadio de Malabo]=NF2
MSHINDI WA 3
Jumamosi Februari 7
2100 Aliefungwa NF1 v Aliefungwa NF2 [Nuevo Estadio de Malabo]
FAINALI
Jumapili Februari 8
2200 Mshindi NF1 v Mshindi NF2 [Estadio de Bata]
Chapisha Maoni