YANGA leo hii imeibuka na ushindi wa bao 1-0 bao ambalo limefungwa na Danny Mrwanda dakika ya 42
Kipindi cha kwanza kilionekana kuwa ni ‘mali’
ya Yanga ambayo ilishambulia zaidi lakini wachezaji wake walipoteza nafasi nzuri
kufunga.
Kipindi cha pili, Polisi wakaonekana
kuimarika na kushambulia zaidi ingawa nao hawakuwa makini katikam ufungaji.
Mliberia, Kpah Sherman naye alionekana kuwa
mwiba kwa mabeki wa Polisi.
Hata hivyo beki mkongwe, Lulanga Mapunda aliongoza vizuri safu yake ulinzi ya Polisi kuhakikisha hairuhusu bao tena.
RATIBA YA KESHO JUMAPILI
16:00 | AZAM FC | Vs | SIMBA SC |
16:00 | KAGERA SUGAR | Vs | NDANDA |
16:00 | STAND UNITED | Vs | COASTAL UNION |
16:00 | MBEYA CITY | Vs | T.PRISONS |
16:00 | RUVU SHOOTING | Vs | MTIBWA SUGAR |
16:00 | JKT RUVU | Vs | MGAMBO JKT |
Chapisha Maoni