Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


 
Michuano ya soka ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON, inaendelea Jumatano leo katika hatua ya nusu fainali kwa Ivory Coast kupambana na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Katika michezo yao ya robo fainali, Ivory Coast iliwasambaratisha Algeria, kwa mabao 3-1. Algeria ni timu nambari moja kwa viwango vya ubora vya Fifa barani Afrika. Nayo Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo iliwaadhibu majirani zao Congo kwa magoli 4-2.
Kiungo wa timu ya Ivory Coast Cheik Tiote huenda akacheza mechi ya leo baada ya kupona maumivu ya kifundo cha mguu, ambayo yalisababisha akose mechi mbili za mwisho za timu hiyo.
Kocha wa Ivory Coast, Herve Renard amesema: "Tiote ameanza mazoezi mepesi. Itakuwa vigumu kwake kuanza mchezo, lakini ameorodheshwa katika kikosi cha leo."
Naye kocha wa DR Congo Florent Ibenge amesema hatapenda kumfanyia majaribio ya kucheza mechi dhidi ya Ivory Coast, nahodha Youssouf Mulumbu, ambaye kocha wake amesema amepona kwa asilimia "70%".
Mlinzi wa DR Congo Gabriel Zakuani hayumo katika kikosi cha leo baada ya kuumia kifundo cha mguu walipocheza dhidi ya Congo.
Alhamisi ni mtifuano mwingine wa nusu fainali kati ya wenyeji Equatorial Guinea dhidi ya Ghana. Kutinga hatua ya nusu fainali Equatorial Guinea waliwang'oa Tunisia inayoshika nafasi ya pili kwa ubora barani Afrika kwa mabao 2-1, huku Ghana ikiichakaza Guinea magoli 3-0.


Chapisha Maoni