Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



>>TOKA DRFA: LIGI MKOA MAKUNDI, RATIBA VYATAJWA!
SOMA ZAIDI:
Release No. 017*
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI*
 *Februari 6, 2015*
 *KAMATI YA NIDHAMU YAWAADHIBU NYOSO, MORRIS*
TFF-LOGO-NEWKamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
imewafungia kati ya mechi tatu na nane wachezaji Juma Nyoso wa Mbeya City
na Aggrey Morris wa Azam kutokana na makosa ya kinidhamu waliyoyafanya
wakiwa uwanjani.
Nyoso ambaye alilalamikiwa na TFF kwa kumfanyia vitendo vya udhalilishaji
mshambuliaji Elias Maguri wa Simba amefungiwa mechi nane za Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL). Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Ibara ya 57 na Ibara ya
11 (f) ya Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012.
Akiwa mbele ya Kamati hiyo jana (Februari 5 mwaka huu) jijini Dar es
Salaam, Nyoso alikiri kufanya na kujutia kosa hilo, pia amemuomba radhi
mchezaji Maguri kwa kitendo hicho.
Akisoma uamuzi huo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wakili Jerome Msemwa
alisema kitendo kilichofanywa na Nyoso ni kosa kubwa, kudhalilisha utu wa
mtu, na ni mfano mbaya kwa watoto na jamii nzima ya mpira wa miguu.
Naye Morris amefungiwa mechi tatu za VPL baada ya kutiwa hatiani kwa
kumpiga mshambuliaji Emmanuel Okwi wakati timu hizo zilipopambana kwenye
mechi ya ligi iliyochezwa Januari 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Kabla ya kusoma uamuzi, Wakili Msemwa alisema mlalamikiwa Morris alikiri
kugongana na Okwi, kwa maelezo kuwa aliingia kwenye 'reli' ndiyo ukatokea
mgongano huo.
Kamati baada ya kupitia malalamiko ya klabu ya Simba, ripoti za Brain CT
scan kutoka Besta Diagnostic Centre na nyingine kutoka Taasisi ya Mifupa
Muhimbili (MOI), taarifa za madaktari zilionyesha Okwi aligongwa kichwani
akiwa anacheza mpira na kuzimia kwa dakika tano, pia mkanda wa video
uliowasilishwa na TFF imeona kulikuwa na kugongana kati ya wachezaji hao.  Hivyo, Kamati ikamtia hatiani Morris kwa kutumia Ibara ya 48(1)(d) ya
Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012 kwa kumfungia mechi hizo tatu na
kumpa onyo kali.
Pia Kamati hiyo imemfungia miezi sita na kumpiga faini ya sh. 200,000
Meneja Vifaa (Kit Manager) wa timu ya Polisi Mara, Clement Kajeri kwa
kuhamamisha vurugu na kuwapiga waamuzi kwenye mechi dhidi ya Mwadui
iliyochezwa Uwanja wa Karume mjini Musoma. Adhabu hiyo imetolewa kwa
kuzingatia kanuni ya 40(2) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Wachezaji watatu wa Friends Rangers; Mahmoud Othman, Khalid Twahil na John
Alexander wamefungia miezi sita na faini ya sh. 500,000 kila mmoja kwa
kumpiga mwamuzi kwenye mechi ya Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya Majimaji.
Licha ya wachezaji hao kuitikia mwito wa Kamati, wachezaji hao walizuiwa na
viongozi wa kuingia ukumbini wakati malalamiko dhidi yao yalipoanza
kusikilizwa. Hatua hiyo iliifanya Kamati ifanye uamuzi baada ya kuusikiliza
upande wa walalamikaji pekee.
Shauri dhidi ya mchezaji George Michael wa Ruvu Shooting kwa kumchezea
ubabe Amisi Tambwe wa Yanga, Kamati imeliahirisha baada ya mlalamikiwa
kupata udhuru uliosababisha asiwepo.
Pia Kamati ya Nidhamu imeelekeza malalamiko ya timu ya Friends Rangers
kupinga refa kuchezesha mechi yao dhidi ya Majimaji kwenye mvua kubwa,
kutoa maamuzi yasiyo halali na kutokuwepo na ukweli kwenye ripoti ya
Kamishna yakasikilizwe na Bodi ya Ligi kwa vile si masuala ya kinidhamu.


TOKA DRFA:
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI            
Release No.05
Februari,06
Chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA,kimetaja makundi ya timu zitakazoshiriki kucheza hatua ya 18 bora (hatua ya pili) ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam,inayotarajia kuanza kutimua vumbi mapema mwezi huu.
Katika kundi (A) limepangwa kuwa na timu za Simba U20,Red Coast,Sifa UTD,Shababi,Ukonga UTD,Zakhem,Ugimbi,Beira hotspurs na Pan Africa.
Katika kundi (B) litakuwa na timu za Yanga U20,Stakishari,FFU,New Kunduchi,Sinza Stars,Changanyikeni,Tuamoyo,Sifapilitan na Azania Unga.
Ligi hiyo ya mkoa wa Dar es salaam iliyokuwa na jumla ya timu 36,imeingia katika hatua ya pili,ambayo  itaanza Februari 11 mwaka huu katika viwanja mbalimbali ,ambapo kwa upande wa
KUNDI (A)  
Simba U20 vs Red Coast       (Karume)
Sifa UTD  vs   Shababi          (Mwl/Nyerere)
Ukonga UTD vs Zakhem           (Airwing)
Ugimbi  vs  Beirahospurs  (Bandari)
KATIKA KUNDI (B) Februari 12
Yanga U20 vs Stakishari          (Karume)
FFU vs New Kunduchi   (Benjamini Mkapa)
Sinza Stars vs Changanyikeni   (Kines)
Tuamoyo vs Sifapolitan          (Bandari)
Viongozi wa DRFA bado wanatoa wito kwa viongozi wa vilabu mbalimbali,mashabiki na wakazi wa jiji pamoja na maeneo ya jirani,kujitokeza kwa wingi kushuhudia vipaji vya wachezaji.
Imetolewa na DRFA
Omary Katanga
Mkuu wa Idara ya Habari (DRFA)


Chapisha Maoni