Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




 The Real Madrid players celebrate their 2-0 Champions League victory against Schalke




Cristiano Ronaldo has now scored 58 Champions League goals in 58 games for Real Madrid
Cristiano Ronaldo has now scored 58 Champions League goals in 58 games for Real Madrid



Cristiano Ronaldo wa Real Madrid akishngilia bao lake katika mchezo wa ligi ya mabingwa kati ya Real Madrid na Schalke uliomalizika kwa Real Madrid kushinda 2-0
Michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, hatua ya kumi na sita bora, iliendelea Jumatano usiku kwa kuzikutanisha timu za FC Basel ya Uswisi na FC Porto ya Ureno katika mchezo ambao FC Basel ndio waliokuwa wenyeji na mchezo wa pili ukiwa kati ya wenyeji Schalke 04 ya Ujerumani dhidi ya mabingwa watetezi Real Madrid ya Hispania.
Tuanze na mchezo wa FC Basel dhidi ya FC Porto. Mpambano huo ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1. Wenyeji FC Basel ndio waliokuwa wa kwanza kujipatia goli katika dakika ya 11 likifungwa na Gonzalez ambalo lilidumu hadi kipindi cha pili, FC Porto waliposawazisha katika dakika ya 75 kwa mkwaju wa penalti iliyofungwa na Danilo baada ya mchezaji wa FC Basel Samuel Walter kuunawa.
Katika mchezo huo ambao ulitawaliwa kwa kiasi kikubwa na wageni, FC Porto wakimiliki kwa asilimia 63% huku wenyeji wakiwa na asilimia 37% ulimalizika kwa mwamuzi wa mchezo huo Clattenburg kuwaonya wachezaji tisa kwa kadi za njano, watano wakiwa ni wa FC Basel na wanne kutoka FC Porto.


Chapisha Maoni