Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.





Mechi no.117 iliyowakutanisha Simba na Yanga katika uwanja wa Taifa, imeingiza jumla ya sh. milioni 436,756,000 kutokana na idadi ya watazamaji 49,758 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo.

Watazamaji 309 walikata tiketi za VIP A, 1,310 VIP B, 1,533 VIP C, Rangi ya Machungwa (Orange) 9,913 huku viti vya rangi ya bluu na kijani wakiingia watazamaji 36,693.

Mgawanyo wa mapato ya mchezo huo ni VAT 18% sh.66,623.796, FDF timu mwenyeji sh. 17,415,300, FDF TFF sh.7,463,700, Gharama za tiketi sh.11,669,600.

Mgao wa Uwanja sh. 50,037,540.51, Gharama za mchezo sh.28,354,606.29, Bodi ya Ligi (TPLB) sh. 26,686,688.27, TFF sh.20,015,016.20, DRFA sh. 11,675,426.12, klabu ya Simba sh. 115,086,343 (34.5%) huku Yanga wakipata sh.81,727.83 (24.5%)


Chapisha Maoni