Mechi
ya Kombe la Shirikisho Barani
Afrika kati ya Yanga dhidi ya FC Platinum ya Zimbambwe kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam, Jumapili imeingiza Sh 91,660,000.
Kitita hicho cha Sh milioni 91 kimetokana na watazamaji 14,563 waliokata tiketi
kushuhudia mchezo huo.
Yanga iliwakung'uta Wazimbabwe hao kwa mabao 5-1 katika mechi hiyo ya kwanza ya Kombe la Shirikisho.
Mgawanyo:
Mgawanyo wa mapato katika mchezo huo ni,
VAT 18% Sh 13,982,033, Gharama ya tiketi Sh 12,380,000, Uwanja 15% Sh 9,794,694.92, Gharama za mchezo 15% Sh 9,794,694.92, TFF 5% Sh 3,264,898.31,
CAF 5% Sh 3,264,898.31 na Yanga 60% Sh 39.178,779.66 (baada ya 18% ya vat kuondolewa).
IMETOLEWA NA MSEMAJI SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA (TFF), BARAKA KIZUGUTO.
Chapisha Maoni