Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


 
Septemba 25 mwaka 2010 Yanga iliibuka na ushindi wa magoli 2-0 katika mechi ya mzunguko wa kwanza na zilirudiana februari 28 mwaka 2011 ambapo Yanga ikashinda tena goli 1-0, mechi zote mbili zilipigwa uwanja wa Taifa.
Msimu uliofuata (2011/2012), mechi ya mzunguko wa kwanza ilichezwa septemba 11 mwaka 2011 na timu hizo zilitoka sare ya 1-1. Mechi ya mzunguko wa pili ilichezwa februari 12 mwaka 2012 na kushuhudia Yanga ikiibuka na ushindi wa goli 1-0. Mechi zote zilichezwa uwanja wa Taifa.
Msimu wa 2012/2013 Yanga iliibuka kidedea kwa magoli 3-2 dhidi ya Ruvu Shooting katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyopigwa Oktoba 20 mwaka 2012. Mechi ya mzunguko wa pili ilipigwa machi 16 mwaka 2013 na Yanga wakashinda tena goli 1-0. Mechi zote zilipigwa uwanja wa Taifa.
Msimu wa mwaka 2013/2014 Yanga walishinda goli 1-0 katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa Oktoba 28 mwaka 2013 na mechi ya marudiano ikapigwa februari 22 mwaka 2014 ambapo Ruvu Shooting walishushiwa mvua kubwa ya magoli 7-0.
Msimu huu mechi ya kwanza ilipigwa januari 18 uwanja wa Taifa na timu hizo kutoka suluhu (0-0).
Hii ndio ilikuwa mechi pekee ambayo nyavu za Ruvu Shooting hazikuguswa, pia Yanga hawakufunga goli.
Ruvu Shooting wanaotumia uwanja wa Taifa kama uwanja wa nyumbani pale wanapocheza dhidi ya Yanga na Simba hawajawahi kushinda dhidi ya Yanga uwanjani hapo kwa miaka mitano sasa.
Hii ni timu ya pili kufungwa magoli mengi zaidi kwa misimu miwili kwani tayari Coastal Union wamevunja rekodi ya msimu uliopita baada ya kufungwa na Yanga 8-0 msimu huu.
Vipigo vyote viwili (7-0 dhidi ya Ruvu Shooting na 8-0 dhidi ya Coastal Union) vimetolewa na kocha mmoja wa Yanga, Hans van der Pluijm.
Yanga wameshinda mechi 7, sare 2 na hawajafungwa mechi yoyote. Wamefunga magoli 17 na kufungwa 3. Tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ni 14 na wamevuna jumla ya pointi 23.
Ruvu Shooting wamefungwa mechi 7 na kutoa sare 2. Wamefunga magoli 3, wamefungwa 17, tofauti ni -14, wamevuna pointi 2 tu.


Chapisha Maoni