Jumanne
Usiku Robo Fainali za UEFA CHAMPIONZ LIGI zitaanza kwa Mechi mbili na moja ikiwa huko Jiji la Madrid,
Spain ndani ya Estadio Vicente Calderon wakati Atletico Madrid watakapokuwa
Wenyeji wa Mahasimu wao Real Madrid.
Mechi hii,
Dabi ya Madrid, maarufu kama El Derbi Madrileño, ni Marudio ya Fainali ya Msimu
uliopita ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambayo Real Madrid waliinyuka Atletico Madrid
Bao 4-1 na kutwaa Ubingwa wa Ulaya kwa mara ya 10.
Mechi
nyingine ya Jumanne Usiku itachezwa huko Jiji la Turin Nchini Italy wakati
Wenyeji Juventus watakapoivaa AS Monaco ya France.
TATHMINI
Kila Timu
itaingia kwenye Mechi hii ikidhamiria kisasi.
Kwa Atletico,
kisasi chao ni kile cha kufungwa na Real kwenye Fainali ya Mashindano haya huko
Lisbon Msimu uliopita na kwa Real ni kubondwa mara 4 na Sare 2 na Atletico
tangu Fainali hiyo.
Vipigo kwa
Real ni pamoja na kutupwa nje ya Spain Supercup na Copa del Rey.
Katika
pambano lao la mwisho Mwezi Februari, kwenye Mechi ya La Liga, Atletico
iliitwanga Real 4-0 ikiwa ndio ushindi wao mkubwa dhidi ya Wapinzani wao
wakubwa katika Miaka 28.
Hilo
limemfanya Kocha wa Real, Carlo Ancelotti, aseme: "Matokeo ya mwisho na
Atletico ndio yanatupa motisha sisi!"
Lakini,
tofauti na Mechi zilizopita Msimu huu, safari hii Real watatinga kwa maadui zao
Vicente Calderon wakiwa na Kikosi kamili kwa mara ya kwanza katika Miezi
Mitano.
James
Rodriguez na Toni Kroos, ambao waliikosa Mechi ya La Liga ya Jumamosi
walipoifunga Eibar 3-0 baada ya kuwa Kifungoni, wanarejea dimbani.
Nao Atletico
wana habari njema ya kurejea dimbani baada ya kuzikosa Mechi mbili akijiuguza
Enka kwa Straika wao Mario Mandzukic ambae tangu ahamie Atletico akitoka
Bayern Munich mwanzoni mwa Msimu amepachika Bao 20 zikiwemo Bao 2 katika
Gemu mbili dhidi ya Real Uwanjani Vicente Calderon.
Jumatano pia
zipo mechi mbili nyingine za Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kati ya PSG na
Barcelona huko Mjini Paris na nyingine itachezwa huko Ureno kati ya FC Porto na
Bayern Munich.
VIKOSI
VINATARAJIWA:
Atletico
Madrid: Oblak; Juanfran, Miranda, Godín, Gámez; Arda Turan, Tiago, Suárez,
Koke; Griezmann, Mandžukić.
Real Madrid:
Casillas; Carvajal, Pepe, Ramos, Marcelo; Kroos, Modrić, James; Bale, Benzema,
Ronaldo.
REFA:
Milorad Mažić (Serbia)
UEFA
CHAMPIONZ LIGI
Robo
Fainali-Mechi za Kwanza
Mechi zote
kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku, Saa za Bongo
Jumanne
Aprili 14
Atlético
Madrid v Real Madrid
Refa:
Milorad Mažić (Serbia) – Uwanja: Estadio Vicente Calderón, Madrid, Spain
Juventus v
AS Monaco
Refa: Pavel
Královec (Czech Republic) – Uwanja: Juventus Stadium, Turin, Italy
Jumatano
Aprili 15
Paris
Saint-Germain v Barcelona
Refa: Bado
kujulishwa– Uwanja: Parc des Princes, Paris, France
FC Porto v
Bayern Munich
Refa: Bado
kujulishwa – Uwanja: Estádio do Dragão, Porto, Portugal
UEFA
CHAMPIONZ LIGI
Robo
Fainali-Mechi za Marudiano
Mechi zote
kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku, Saa za Bongo
Jumanne
Aprili 21
Bayern
Munich v FC Porto [Allianz Arena, Munich, Germany]
Barcelona v
Paris Saint-Germain [Nou Camp, Barcelona, Spain]
Jumatano
Aprili 22
Real Madrid
v Atletico Madrid [Santiago Bernabeu, Madrid, Spain]
AS Monaco v
Juventus [Stade Louis II, Monaco, France]
Chapisha Maoni