Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



Neymar mshangiliaji

Neymar jukwaani 1Thiago Silva aliyenyang’anywa unahodha wa Brazil alianza kuifungia Brazil goli la kwanza zikiwa zimepita dakika tisa tu tangu kuanza kwa mchezo, lakini dakika ya 51 Roberto Firmino akaihakikishia Brazil kufuzu kucheza hatua ya robo fainali baada ya kuifungia timu yake goli la pili akimalizia kazi safi iliyofanywa na Wllian.
Thiago SilvaGoli la kufutia machozi la Venezuela lilifungwa na Miku dakika ya 84 ya  mchezolakini lilikua halina msaada kwa timu yake ambayo imemaliza mkiani kwenye kundi C ikiwa na ponti tatu.
Brazil itakutana na Paraguay kwenye mchezo wake wa robo fainali utakaopigwa siku ya Jumamosi mchezo ambao unatarajiwa kuwa na upinzani mkali na wenyekuvutia.
Mchezo mwingine wa kundi C uliopigwa jana usiku ulikuwa  kati ya Colombia dhidi ya Peru, mchezo huo ulimalizika kwa timu hizo kwenda sare ya bila kufungana ambapo Falcao bado ameonekana kushindwa kurejesha makali yake ya kupasia nyavu.


Chapisha Maoni