Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


 
Nyota mkubwa na nahodha wa Argentina, Lionel Messi ameonya wenzake ni lazima washinde mechi yao dhidi ya mabingwa Uruguay katika kipute cha Copa Amerika Jumanne kesho ili kuendeleza ndoto yao ya kubeba taji hilo. 

Argentina ambao ni chaguo la wengi kunyakua taji hilo walipata mshtuko wakati Paraguay walijiinua kutoka 2-0 nyuma kulazimisha sare ya 2-2 katika mechi yao ya kwanza Kundi B. 

“Kuongoza 2-0 na kuishia na sare ya 2-2 kwanikera. Tukiangalia mambo sasa, mechi ya Uruguay ni lazima tuishinde,” Messi alizidi.
Uruguay walianza kampeni yao kwa kusitasita kuwaondoa wanyongwe waalikwa Jamaica 1-0 huku Messi na wenzake watakao funga mechi za makundi na wana Reggae Boys wakilenga kuibuka timu bora kwa kuwalaza Uruguay. 

“Katika kipindi cha kwanza, tulidhibiti mchezo, tulibuni nafasi na kufunga. Mambo yote yalibadilika katika kipindi cha pili walipoanza kucheza vyema zaidi,” nyota huyo wa Barcelona aliendelea. 

“Tulistahili kuweka mpira miguuni yetu,” Messi aliendelea.


Chapisha Maoni