Na Ally Ruambo.
TIMU
ya Vijana chini ya miaka 12 kutoka wilayani kilwa wanatarajiwa kuondoka nchini kuelekea nchini
Finland kushiriki katika mashindano ya
mpira wa miguu(min football) yanayojumuisha vijana chini ya miaka kumi na
mbili.
Mashindano
hayo ambayo hufanyika nchini finland kila
mwaka ambapo wilaya moja nchini Tanzania huchaguliwa kuunda timu ambayo inaenda
kuiwakilkisha nchi katika mashindano hayo
nchini finland.
Wachezaji
hao kumi na mbili wanaounda timu hiyo wamepatikana katika mchujo ambao
ulikutanisha wanafunzi mbali mbali toka shule tofauti za msingi kutoka wilayani
hapo chini ya mpango unaojulikana kwa jina la ELIMU NA MICHEZO ambapo FC VITO
kutoka nchini finland kwa kushirikiana na wizara ya elimu Tanzania wanaratibu
mpango huo.
Timu hiyo inaenda kushindana katika mchezo
ambao unajulikana kama min football ambao unakua tofauti kidogo na mpira wa
miguu amabao tumeuzoea ambapo idadi ya wachezaji wa ndani wanakua pungufu, wanakua
7 pia vipimo vya uwanja vinapungua ukilinganisha na mpira wa miguu wa kawiada.
Timu ya vijana chini ya miaka
kumi na mbili kutoka wilaya ya kilwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara
baada ya kukabidhiwa bendera ya nchi.
|
Akizungumza
na mwandishi wetu afisa michezo wilaya ya kilwa ndugu Mtule amesema timu iko
katika hali mzuri imefanya maandalizi ya kutosha na vijana wana morali ya
mashindano na anaamini watafanya vizuri.
“Vijana walikua wengi
ambao wana viwango vizuri lakini tumewaacha kwa kigezo cha umri kwa
sababu wana umri ambao umezidi miaka
kumi na mbili kitu ambacho ni kinyume na kanuni za mashindano ambapo wachezaji
wanaotakiwa ni chini ya umri wa miaka kumi na mbili pia walikua wengi lakini
waliokua wanahitajika ni kumi na mbili tu.” Alisema Mtule.
Pia
ameongeza kua wamekumbana na changamoto nyingi lakini changamoto kubwa ni baadhi ya wazazi wachache hawakua tayari
kuwapa ruksa watoto wao kwa safari ya kuelekea finland mara baada ya
kuchaguliwa kwahiyo wakaamua kuwaacha
na kuwachagua wengine ambao wana uwezo na wako tayari kwa safari.
Kwa
upande wa wachezaji wamesema wako vizuri kwani wamefanya mazoezi ya kutosha
kwahiyo wanakwenda nchini finland kushindana na kuhakikisha wanarudi na ushindi
kwa taifa letu.
Mapema
jana vijana hao walikabidhiwa bendera ya nchi na mkuu wa wilaya ,wilaya ya
kilwa Mh. ABDALLAH ULEGA Katika hafla fupi ya kuiaga timu hiyo iliofanyika katika viunga vya majengo ya halmashauri ya wilaya ya
kilwa ambapo viongozi kutoka idara mbali
mbali,viongozi wa dini, kamati ya ulinzi na usalama ,wanafunzi pamoja na ndugu
na jamaa wa wachezaji hao wali udhuria katika hafla hiyo.
Msafara
wa timu hiyo pamoja na afisa michezo wa wilaya
umeanza safari leo alfajiri
kutoka kilwa kuelekea jijini dare s
salaam ambapo mara baada ya kufika dar es salaam watatembelea ubalozi wa finland nchini tanzania kabla ya kuanza safari kuelekea nchini
finland mapema wiki hii ambako mashindano yanatarajia kufanyika.
Mdau mkubwa wa michezo wilayani
kilwa Hamisi Kassinge kataka picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji.
|
Chapisha Maoni