TAARIFA:Kipa waManchester United David De Gea hatacheza dhidi ya Tottenham hapo Kesho huku akiendelea kuhusishwa na kuhamia Real Madrid.
Kwa kipindi chote hiki kuelekea Msimu mpya ambao unaanza Kesho kwa hiyo Mechi Uwanjani Old Trafford, De Gea, mwenye Miaka 24, ametajwa sana kutaka kurudi kwao Spain kuichezea Real.
Akiongelea Mechi hii ya kwanza, Meneja wa Man United, Louis van Gaal, amesema: “Namfikiria yeye kama binadamu na si Mchezaji. Naona hatamudu haya.”
Kukosekana kwa De Gea kunaweza kufungua njia kwa Kipa mpya wa Kimataifa wa Argentina, Sergio Ramos, kucheza Mechi yake ya kwanza kabisa.
Kipa mwingine wa Man United ni Kipa wa zamani wa Barcelona, Victor Valdes, mwenye Miaka 33, lakini nae ametemwa kwenye Kikosi cha Kwanza na yumo kwenye Listi ya Wachezaji wanaouzwa baada ya kufarakana na Van Gaal.
WAKATI HUO HUO
Manchester United imethibitisha kuuzwa kwa Fowadi wao Angel Di Maria kwa Paris Saint-Germain ya France.
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Argentina alisainiwa na Man United Mwaka Jana kutoka Real Madrid kwa Dau la Rekodi ya Uingereza na aliichezea Mechi 24 huku 8 akitokea Benchi.
Akiwa na Man United, Di Maria alifunga Bao 4.
Chapisha Maoni