Siku
chache baada ya kutwaa ubingwa wa Uefa Super Cup, Barcelona wamekiona
cha moto baada ya kukutana na kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Athletic
Bilbao.
Licha ya kuwemo kwa nyota Lionel Messi, Bilbao wametoa adhabu hiyo kwa Barcelona katika mechi ya Super Cup ya Hispania.
Hadi mapumziko, Bilbao walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Mikel San Jose aliyefunga katika dakika ya 13.
Huku
ikionekana Barcelona ingerejea na kujirekebisha katika kipindi cha pili
kama ilivyofanya kwenye mechi ya Uefa Super Cup dhidi ya Sevilla baada
ya kutangulia kufungwa na kusawazisha, haikuwa hivyo.
Kwani
Bilbao ndiyo walizidi kupaa na kufunga mabao ya harakaharaka baada ya
Artiz Aduriz kufanya mabao mawili ya fasta katika dakika ya 53 na
baadaye 63.
Kitendo
cha Bilbao kufikisha mabao matatu kilionekana kuwachanganya Barcelona,
wakaendelea kushambulia mfululizo na kujisahau kufanya ulinzi mzuri.
Hali hiyo ilisababisha Bilbao kupata bao la nne kupitia Aduriz aliyekuwa anafunga lake la tatu au hat trick.
Chapisha Maoni