Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Kikosi cha Azam FC
kimeendeleza ushindi katika
Ligi Kuu Bara baada ya
kushinda kwa mabao 2-1 dhidi
ya Mbeya City katika mechi
iliyopigwa kwenye Uwanja wa
Azam Complex, Chamazi
jijini Dar es Salaam.
Azam ilianza Ligi Kuu Bara
kwa kuichaa Prisons bao
2-1, ikaendeleza kipigo cha
2-0 kwa Stand United kabla
ya kuitandika Mwadui FC
1-0.
Sasa ina pointi 12 sawa na
Yanga na Mtibwa Sugar
ambazo hazijapoteza hata
mechi moja katika nne
zilizocheza.
Mabao ya Azam FC katika
mchezo huo yalifungwa na
kiungo Mudathir Yahya
katika dakika ya 11 kabla
ya Kipre Tchetche kumaliza
kazi katika dakika ya 52.
Hata hivyo, Mbeya City
walijitutumua na kupata bao
katika dakika ya 55 kupitia
kiungo wao Raphael Alpha.
Hata hivyo, dakika za
mwisho Mbeya City
walionekana kukaa vizuri
zaidi na kuwahenyesha Azam
FC ambao hata hivyo safu
yao ya ulinzi ikiongozwa na
Serge Wawa ilionekana
kusimama imara.

LIGI KUU VODACOM
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Septemba 26
Simba 0 Yanga 2
Coastal Union 0 Mwadui 0
Tanzania Prisons 1 Mgambo Shooting 0
JKT Ruvu 0 Stand United 1
Mtibwa Sugar 1 Majimjaji 0
Kagera Sugar v Toto Africans (Uwanja wa Ali
Hassan Mwinyi, Tabora)



Chapisha Maoni