Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


MALINZI AZINDUA KAMBI YA U-13
WATAKAOCHEZA FAINALI U-17 ZA
AFRIKA 2019 NCHINI TANZANIA!
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini
(TFF), Jamal Malinzi leo amezindua rasmi kambi
ya kikosi cha timu ya Taifa umri chini ya miaka
13 ambacho kitakua pamoja kuelekea fainali za
Afrika za vijana umri chini ya miaka 17 (U17)
zitakazofanyika nchini Tanzania mwaka 2019.
Kikosi hicho ni cha vijana 20 ambao waliteuliwa
tokana na mashindano ya vijana ya umri chini ya
miaka 13 (U13) yaliyofanyika Mwanza mwezi Juni
mwaka huu.
Malinzi amezindua kambi hiyo itakayodumu kwa
muda wa miaka mitano hadi mwaka 2019. Kambi
hiyo itakuwa kwenye shule ya kulea na kukuza
vipaji vya mpira ya Alliance iliyopo jijini Mwanza.
Wakiwa Alliance vijana hao gharama za masomo,
matunzo na vifaa zitatolewa na Shirikisho la
Mpira wa Miguu nchini (TFF).
Akizindua kambi hiyo Malinzi aliongea na wazazi
wa watoto hao na kuwaahidi kuwa TFF kwa
kushirikiana na shule ya Alliance itahakikisha
vijana hao wanapewa elimu nzuri itakayozingatia
maadili.
Wazazi wa watoto wametoa shukrani kwa uteuzi
huu wa watoto wao na Mkurugenzi wa shule ya
Alliance Bw James Bwire ameahidi kutoa elimu
bora na mafunzo mazuri kwa vijana.
Jumla ya vijana 455 toka mikoa yote ya Tanzania
walishiriki mashindano hayo.
IMETOLEWA NA TFF



Chapisha Maoni