Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


MIMI ni Mtanzania kama
wengine zaidi ya milioni 45
ambao tunaishi katika nchi
yenye utajiri mkubwa kwa
mambo mengi sana.
Nimezaliwa Tanzania,
nimekulia Tanzania, bado
ninaishi hapa Tanzania,
ninaomba mwisho wa maisha
yangu uishie hapa, nizikwe
katika udongo wa taifa hili
ninalolipenda moyoni.
Kama nimezaliwa, nimekulia,
ninaishi pia ninatamani
kuzikwa hapa Tanzania.
Basi ninaamini sina sehemu
nyingine ninayoweza
kuitetea, kuigombania kwa
nguvu zangu zote zaidi ya
nchi yangu.
Mimi ni Mtanzania ambaye
nimekuwa nikijiuliza mengi
kwa sasa. Kwamba kama
uchaguzi wa keshokutwa
usipokuwa salama,
nitakimbilia wapi kwa kuwa
sehemu ninaipenda kuliko
zote kwa ajili ya kuishi ni
hapa Tanzania.
Ndiyo maana nimekuwa
nikipambana kueneza ujumbe
wa amani kuhakikisha
Tanzania inapita salama
katika kipindi hiki kigumu
bila ya kujali Watanzania
wanamtaka huyu au yule,
lakini kikubwa wachague kwa
amani.
Timu yetu ya taifa, Taifa
Stars ina kibarua kigumu
kuwania kuchea Kombe la
Dunia na Novemba 14
itakutana na Algeria jijini
Dar es Salaam. Baada ya
hapo, siku chache tu yaani
Novemba 17, Stars itakuwa
nchini Algeria kupambana na
wenyeji.
Utaona ni mzigo mkubwa kwa
Stars ambao hawajawahi
kuupata huenda zaidi ya
miaka 10 iliyopita.
Nitakueleza kwa nini.
Kwanza Algeria, ndiyo timu
bora barani Afrika kwa
ubora wa viwango katika
kipindi hiki. Algeria ni
namba moja Afrika, inashika
namba …..dunia. Tanzania ni
namba …..Afrika, duniani ni
namba……
Pili; Algeria ndiyo timu
bora ya Afrika wakati wa
michuano ya Kombe la Dunia
2014 iliyofanyika nchini
Brazil.
Tatu; tunakutana na timu
iliyoshiriki Kombe la Dunia
zaidi ya mara moja.
Unapozungumzia mbinu za
kufuzu, watakuwa wanazijua.
Ukizungumzia wafanye nini
kwa wakati gani, wanajua
zaidi ya sisi.
Nne; mechi zipo karibu
sana. Tofauti ya siku tatu,
kucheza na kusafiri, si
kitu kidogo. Je, kwa
wachezaji wetu wanaliweza
hilo? Kuna mambo mengi sana
ya kujiuliza.
Lazima tukubali kila
Mtanzania atakuwa anataka
kuiona Stars inafuzu.
Lazima tukubaliane huu
ndiyo wakati suala la
utaifa linapaswa kuonekana
zaidi kuliko wakati
mwingine.
Mimi nimekuwa kati ya wale
wanaokosoa sana katika
suala la utekelezaji wa
Taifa Stars. Safari hii
nimejumuishwa katika kamati
za kuisaidia Taifa Stars
ishinde. Mimi ni mwenyekiti
wa kamati ya uhamisishaji.
Lengo la kamati ni
kuwahamasisha Watanzania
kwa wingi kujitokeza
uwanjani siku ya mechi.
Naona hili linawezekana
ndiyo maana nimetaka
kuwakumbusha kwamba
hakutakuwa na mafanikio
kama tutatumia muda huu
kulumbana sana.
Kamati hizi, hakuna
maslahi, hazina hata bajeti
ya fedha kwamba kuna watu
wanafaidika. Hadi sasa
karibu kila mjumbe anatumia
muda na wakati mwingine
fedha zake kuhakikisha
mambo yanakwenda vizuri.
Kuiunga mkono Stars ni
jambo bora zaidi badala ya
kufarakana. Siamini kama
Algeria wamekuwa wakifanya
vema wakiwa wametengana.
Tunaweza kuchagua wenyewe
kwa kipindi hiki, kuonyesha
uzalendo na Tanzania ifanye
vema, jambo ambalo
linawezekana. Au tukae na
kuanza kupasua umoja ili
tufeli.
Atajayefanya hivyo,
hatakuwa Mtanzania mpenda
nchi yake. Sitaki kuwafumba
watu midomo, lakini unaweza
pia kufumba mdomo kwa faida
ya nchi yako katika kipindi
ambacho suala la maslahi ya
taifa linapewa kipaumbele.
Kimaisha, mambo
yanabadilika, lakini suala
la utaifa hata kwa mwenye
uhakika wa kubadilisha
utaifa wake, bado utaifa wa
mwanzo hauwezi kuuondoa
moyoni mwako.
Naipenda nchi yangu ndiyo
maana niko tayari kusaidia.
Wengine pia tuungane,
tukishinda tuwe pamoja,
tukishindwa tubaki pamoja.
Hakuna linaloshindikana
mnapokuwa pamoja.
Wako asiye mwoga
SALEH ALLY



Chapisha Maoni