Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


MSHAMBULIAJI mahiri wa Lipuli ya Iringa Dany Mrwanda atakosa pambano kali kati ya Kurugenzi na timu yake ya Lipuli, kufuatia kutumikia  kadi nyekundu  aliyorambwa hivi karibuni.

Mrwanda alipata  kadi nyekundu katika mechi ya ligi daraja la kwanza baada ya kumchezea faulo kipa wa polisi ya Morogoro, Mchezo ambao Lipuli ilifungwa bao 2-0.

akizungumzia mchezo unaokuja kocha wa Lipuli Peter Mhina amesema licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji  katika kikosi cha kwanza ushindi katika mchezo huo ni lazima.

"mchezo ni mgumu lakini tumejipanga vizuri ili kuvuna pointi tatu muhimu,tuliteleza katika mchezo uliopita lakini tupo tayari kuvuna pointi michezo iliyobakia"alisema Mhina.

Mchezo huu ambao utapigwa katika uwanja wa Mafinga utakuwa mgumu kutokana na upinzani mkali ulioibuka baina ya timu hizo ambapo kila timu inaitaji pointi tatu muhimu.



Chapisha Maoni