Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Jose Mourinho hana wasiwasi na kibarua chake
kama Meneja hata kama Chelsea watamaliza
Msimu huu wakiwa katikati ya Msimamo wa Ligi
Kuu England.
Hivi sasa Chelsea, ambao ndio Mabingwa
Watetezi, wapo Nafasi ya 16 kwenye Ligi baada
ya Mechi 8 ambazo wamefungwa Mechi 4 na huu
ni mwanzo wao mbovu tangu Msimu wa 1978/79.
Lakini
Mourinho, ambae huu ni Mwaka wake wa pili
tangu arejee tena kama Meneja na ambae
mwanzoni mwa Msimu alisaini Mkataba mpya wa
Miaka Minne, amesisitiza hana hatari ya
kufukuzwa.
Alipohojiwa kama ana hakika atabaki kama
Meneja hata kama Chelsea itamaliza Ligi ikiwa
Nafasi za kati, Mourinho alijibu: “Ndio.
Sikuambiwa hivyo kwa sababu sitegemei
tutamaliza nafasi za kati kwenye Msimamo.”
Mara baada ya kuchapwa 3-1 na Southampton
mapema Mwezi huu Uwanjani Stamford Bridge,
Mourinho alisisitiza hataondoka Chelsea labda
afukuzwe na Siku 2 baadae Klabu ya Chelsea
ikatoa tamko kumuunga mkono.
Hatua hiyo ilimfurahisha mno Mourinho na
kusisitiza hilo ni jambo muhimu mno kwake.
Hii Leo Chelsea wako kwao Stamford Bridge
kucheza Mechi ya Ligi Kuu England na Aston Villa
ambao wako Nafasi ya 18 zikiwa ni Nafasi 2
nyuma ya Chelsea wakiwa Pointi 4 nyuma yao.
CHELSEA-Mechi zijazo:
Jumamosi Oktoba 17
Ligi Kuu England
1700 Chelsea v Aston Villa
Jumanne Oktoba 20
UEFA Championz Ligi - Kundi G
2145 Dynamo Kiev v Chelsea
Jumamosi Oktoba 24
Ligi Kuu England
1700 West Ham v Chelsea
Jumanne Oktoba 27
Capital One Cup – Raundi ya 4
2245 Stoke v Chelsea
Jumamosi Oktoba 31
Ligi Kuu England
1545 Chelsea v Liverpool
Jumatano Novemba 4
UEFA Championz Ligi - Kundi G
2245 Chelsea v Dynamo Kiev



Chapisha Maoni