Kwa sasa hawapo tena kwenye
tasnia hii ya soka, lakini mchango wao utabaki katika vitabu vya
historia. Walijitahidi kadri walivyoweza kuhakikisha timu zao
zinafurahia mafaniko iwe kwenye ligi za ndani ama michuano ya Ulaya.
Kutokana na utangulizi huo, hawa ndio wachezaji watano bora ambao
wamewahi kucheza michezo ya UEFA wakiwa na umri mkubwa.
5. Edwin van der Sar–miaka 40 na siku 212
FC Barcelona v Manchester United FC, 28/05/2011
“Mara nyingi unakuwa na ndoto
za kucheza katika timu yako ya taifa lakini vile vile kunyakua ubingwa
wa Ligi ya Mabingwa Ulaya,” alisema.
4. David Weir–Miaka 40 na siku 212
Bursaspor v Rangers FC, 07/12/2010
“Sifikirii kuhusu hilo; nadhani hilo ndio jibu fupi kiukweli,” aliiambia UEFA.com.
“Najifikiria mwenyewe kama moja
ya wachezaji. Sivutiwi na umri wangu lakini nimekuwa nikijibu kuhusu
hilo kwa kipindi kirefu sasa na kuona kwamba suala hili kamwe
halitabadilika.”
3. Alessandro Costacurta-miaka 40 na siku 213
AEK Athens FC v AC Milan 21/11/2006
Alishinda mataji 23 katika
maisha yake ya soka, huku mataji mengi akivuna pindi akiwa na klabu ya
Ac Milan. alicheza michezo 458 akiwa Ressoneri, akishika nafasi ya tatu
miongoni mwa wachezaji waliocheza michezo mingi zaidi klabuni hapo.
Alistaafu akiwa amecheza michezo 660 kunako ligi ya Serie.
2. Mark Schwarzer- miaka 41 na siku 198
Club Atlético de Madrid v Chelsea FC, 22/04/2014
Mchezaji huyu wa zamani wa timu
ya taifa ya Australia alikuwa mchezaji wa kwanza mwenye umri mkubwa
kucheza kwa mara ya kwanza kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Chelsea
ilipoinyuka timu ya Steaua BucureÅŸti bao 1-0.
“Ulikuwa ni mchezo mkubwa sana
kwangu na nimefurahi sana kwa kitendo cha kocha kuniamini na kunipa
nafasi ya kutimiza ndoto za maisha yangu za kucheza Ligi ya Mabingwa
Ulaya,” Schwarzer aliiambia UEFA.com.
1. Marco Ballotta- 43 years and 253 days
Real Madrid CF v SS Lazio, 11/12/2007
“Wakati nikiwa kijana mdogo
niliambiwa kufanya juhudi ili nikuze kiwango; na sasa nina umri mkubwa,
naambiwa kuongeza juhudi kutokana na umri wangu kuwa mkubwa,”
“Hakuna siri juu ya hili.
Unatkiwa kupewa motisha, lakini jambo kubwa zaidi ni kuwa na furaha
wakati wote, iwe mazoezini au kwenye mechi. Kutokuwa na majeraha ya mara
kwa mara, nadhani utapata jibu juu ya hilo.” alisema Marco. Alistaafu
rasmi mwaka 2008.
Chapisha Maoni