Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Nsa Job, mchezaji wa zamani wa vilabu vya
Simba , Yanga na Cosatal Union Baada ya picha nyingi na taarifa kuzagaa
zinazomhusu mchezaji wa zamani wa vilabu vya
Yanga, Simba pamoja na Coastal Union Nsa
Job akiwa amelazwa hospitali kufuatia
kujeruhiwa vibaya na watu wanaodhaniwa kuwa
ni wafuasi wa CHADEMA, imetoka taarifa kuwa
hali yake inaendelea kuwa nzuri. Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa
Kilimanjaro Goodluck Moshi amesema hali ya
Nsa Job anaendelea vizuri akiwa bado
amelazwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi
lakini tayari ameondolewa mashine za
kumsaidia kupumua. “Taarifa iliyopo ni kwamba, alipigwa (Nsa Job)
na jiwe kubwa kichwani wakati akiwa kwenye
gari akitokea nyumbani kwa mgombea ubunge
Manispaa ya Moshi kupitia Chama Cha
Mapinduzi Ndugu Denis Mosha”, Moshi
ametaarifu . “Wakati wanatoka nyumbani kwa Mosha wakiwa
kwenye gari yeye (Nsa Job), Mosha na mtu
mwingine, walipofika barabarani, likarushwa
jiwe kubwa likapita kwenye kioo cha dirisha na
kumpasua kwenye kichwa na taya, akakimbizwa
KCMC amefanyiwa upasuaji bado yupo ICU
lakini hali yake inaendelea vizuri”. “Ameshaondolewa mashine za kupumulia na
anaweza kuongea hivi sasa, ni jambo la
kumshukuru Mungu kutokana na hali halisi
ilivyokuwa imejitokeza”. Jana kuna picha zilienea kwenye mitandao ya
kijamii zikionesha kuwa Nsa Job amelazwa
kwenye wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) baada
ya kujeruhiwa vibaya kwenye eleo la kichwa.


Chapisha Maoni