Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Manchester United, Arsenal na Chelsea ni miongoni mwa Timu 13 ambazo zinagombea Nafasi 7 za kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI katika Mechi za mwisho za Makundi zitakazochezwa Desemba 8 na 9.
Timu 9, ikiwemo Barcelona ambao ndio Mabingwa Watetezi, tayari zimeshafuzu huku Timu 7 zikiwania Nafasi ya 3 ya Makundi yao ili kucheza UEFA EUROPA LIGI wakati tayari zipo Timu 3 zinakamilisha Ratiba tu baada ya kutupwa nje ya Mashindano haya.

TIMU ZILIZOFUZU:
**Bado 7
Real Madrid
Paris Saint-Germain
Atlético Madrid
Benfica
Juventus
Manchester City
Barcelona
Bayern München
Zenit
TIMU ZINAZOWEZA KUFUZU:
Wolfsburg*
Manchester United*
PSV Eindhoven
AS Roma
Bayer Leverkusen
BATE Borisov
Olympiacos*
Arsenal*
FC Porto*
Chelsea*
Dynamo Kyiv*
Gent*
Valencia*
*Zina uhakika wa kumaliza ndani ya 3 Bora
TIMU ZINAZOWEZA KUMALIZA NAFASI YA 3:
Shakhtar Donetsk
Malmö
CSKA Moskva
Galatasaray
Astana
Borussia Mönchengladbach
Sevilla
TIMU ZILIZOTUPWA NJE:
Dinamo Zagreb
Maccabi Tel-Aviv
Lyon
Droo ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UCL na ile ya EUROPA LIGI Raundi ya Mtoano ya Timu 32 itafanyika Desemba 14.

Jumanne Desemba 8
KUNDI: A:
Real Madrid (Pointi 13, Imeshafuzu) v Malmö (3)
Paris Saint-Germain (10, Imeshafuzu) v Shakhtar Donetsk (3)
-Real Madrid washatwaa Ushindi wa Kundi na PSG Nafasi ya Pili.
-Shakhtar lwako mbele ya Malmö kwenye Matokeo ya Uso kwa Uso na hivyo watatwaa Nafasi ya 3 na kucheza EUROPA LIGI wakishinda au wakipata matokeo sawa nay a Malmo.
KUNDI: B:
PSV Eindhoven (Pointi 7) v CSKA Moskva (4)
Wolfsburg (9) v Manchester United (8)
-Wolfsburg watafuzu wakipata Sare na watachukua Nafasi ya Kwanza wakishinda.
-Man United watasonga wakishinda na kuwa Washindi wa Kundi.
-PSV watafuzu wakishinda au wakidroo ikiwa Man United itafungwa
-CSKA watatwaa Nafasi ya 3 wakiifunga PSV.
KUNDI: C:
Benfica (Pointi 10, Imeshafuzu) v Atlético Madrid (10, Imeshafuzu)
Galatasaray (4) v Astana (3)
-Benfica na Atlético wamefuzu na Benfica watakuwa Washindi wa Kwanza wakishinda au kutoka Sare.
-Astana lazima washinde ili kutwaa Nafasi ya 3.
KUNDI: D:
Manchester City (Pointi 9, Imeshafuzu) v Borussia Mönchengladbach (5)
Sevilla (3) v Juventus (11, Imeshafuzu)
-Juventus wataikosa Nafasi ya Kwanza wakifungwa na City kushinda.
-Sevilla watamaliza Nafasi ya 3 wakishinda ikiwa Borussia Mönchengladbach hawatashinda.
Jumatano Desemba 9
KUNDI: E:
Bayer Leverkusen (Pointi 5) v Barcelona (13, Imeshafuzu)
AS Roma (5) v BATE Borisov (4)
-Barcelona wameshatwaa ushindi wa Kundi.
-AS Roma watafuzu wakishinda.
-Bayer Leverkusen wanahitaji kushinda na kuomba AS Roma wasishinde ili wafuzu
-Sare itawapa Leverkusen Nafasi ya 3.
-BATE lazima washinde na kuomba Leverkusen wasishinde ili waendelee kucheza Ulaya.
KUNDI: F:
Olympiacos (Pointi 9) v Arsenal (6)
Dinamo Zagreb (3) v Bayern München (12, Imeshafuzu)
-Bayern ndio Mabingwa wa kundi.
-Olympiacos waliifunga Arsenal 3-2 huko Emirates na hivyo Arsenal wanatakiwa wapate ushindi bora Zaidi ya huo dhidi ya Olympiakos watakapokutana huko Athens.
-Dinamo wako nje.
KUNDI: G:
Chelsea (10) v Porto (10)
Dynamo Kyiv (8) v Maccabi Tel-Aviv (0)
-Mshindi wa Chelsea v Porto ndie Mshindi wa Kundi.
-Chelsea watafuzu kwa Sare.
-Dynamo will be through with a winwatafuzu wakishinda na ikiwa Mechi kati ya Chelsea na FC Porto ni Sare basi Nafasi za Kundi zitaamuliwa kwa tofauti ya Magoli nah ii itawaweka Dynamo Nafasi ya Kwanza, Chelsea ya Pili na FC Porto ya Tatu.
-Maccabi wapo nje.
KUNDI: H:
Gent (7) v Zenit (15, Imeshafuzu)
Valencia (6) v Lyon (1)
-Zenit wameshatwaa Ushindi wa Kundi.
-Gent watafuzu wakishinda au Valencia wasiposhinda.
-Lyon wapo nje.
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Mechi za Mwisho za Makundi
RATIBA
Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku, isipokuwa inapotajwa
Jumanne Desemba 8
KUNDI A
Paris St Germain v Shakhtar Donetsk
Real Madrid v Malmö FF
KUNDI B
PSV v CSKA
VfL Wolfsburg v Man United
KUNDI C
Benfica v Atletico Madrid
Galatasaray v FC Astana
KUNDI D
Man City v Borussia Mönchengladbach
Sevilla v Juventus
Jumatano Desemba 9
KUNDI E
Bayer Leverkusen v Barcelona
Roma v BATE Borislov
KUNDI F
Dinamo Zagreb v Bayern Munich
Olympiakos v Arsenal
KUNDI G
Chelsea v FC Porto
Dynamo Kiev v Maccabi Tel Aviv
KUNDI H
KAA Gent v Zenit Saint Petersburg
Valencia v Lyon

TAREHE MUHIMU:
-Ratiba Mechi za Makundi:
Mechidei 1: 15/16 Septemba
Mechidei 2: 29/30 Septemba
Mechidei 3: 20/21 Oktoba
Mechidei 4: 3/4 Novemba
Mechidei 5: 24/25 Novemba
Mechidei 6: 8/9 Decemba
Raundi za Mtoano:
-Droo ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16: Desemba 14
Mechi Februari 16/17/23/24 na Marudiano Machi 8/9/15/16
-Droo ya Robo Fainali: Machi 18
Mechi Aprili 5/6 na Marudiano Aprili 12/13
-Droo ya Nusu Fainali: Aprili 15
Mechi Aprili 26/27 na Marudiano Mei 3/4
FAINALI
Mei 28
San Siro, Milan, Italy



Chapisha Maoni