HABARI nzito zimevuja kuwa Manchester United imefanya mazungumzo na Wawakilishi wa Jose Mourinho na kwamba imeshakubalika kuwa ataanza kazi rasmi kama Meneja hapo Julai 1.
Meneja wa sasa, Louis van Gaal ana Mkataba na Man United hadi mwishoni mwa Msimu wa 2016/17 lakini hivi sasa mapenzi yake kwa Mashabiki wa Klabu hiyo yametoweka kutokana na Soka bovu na kutokuwa na mtiririko mzuri wa ushindi.
Ripoti zimedai Mtendaji Mkuu wa Man United, Ed Woodward, ameshafanya mazungumzo na Wakala wa Mourinho, Jorge Mendes, ili Mreno huyo apewe kazi.
Inasadikiwa Wamiliki wa Man United, Familia ya Kimarekani ya kina Glazer, imempa uhuru Woodward kumsaini yeyote ambae anafaa kuwa Meneja wa Klabu hiyo.
Kutokana na uhusiano mzuri kati ya Woodward na Mendes, ambae pia aliwawakilisha Angel di Maria na Radamel Falcao waliotua Old Trafford Msimu uliopita na pia kumwakilisha Kipa David de Gea aliesaini Mkataba mpya na Man United Mwezi Septemba wa Miaka 4, zipo kila dalili kuwa Mourinho ndie atakuwa Meneja anaefuata wa Man United.
BPL:
Ratiba
Jumamosi 6 Februari 2016
1545 Man City v Leicester
[Mechi kuanza Saa 12 Jioni]
Aston Villa v Norwich
Liverpool v Sunderland
Newcastle v West Brom
Stoke v Everton
Swansea v Crystal Palace
Tottenham v Watford
Jumapili 7 Februari 2016
1630 Bournemouth v Arsenal
1900 Chelsea v Man United
Jumatatu 8 Februari 2016
2300 Southampton v West Ham
Chapisha Maoni