RATIBA YA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA…
Februari 13, 2016
Stand United Vs Simba SC
Mgambo JKT Vs African Sports
Mbeya City Vs Toto Africans
Ndanda FC Vs Majimaji
JKT Ruvu Vs Kagera Sugar
Februari 14, 2016
Mwadui FC Vs Prisons
Coastal Union Vs Azam FC
Yanga SC itaondoka Jumatano kwenda Mauritius kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika
MECHI mbili za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania za klabu ya Yanga SC dhidi ya Mtibwa Sugar na dhidi ya African Sports zimefutwa na zitapangiwa tarehe nyingine.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto leo amesema kwamba mechi hizo zimefutwa ili kupisha mechi mbili za Yanga SC za Ligi ya Mabingwa Afrika.
Yanga SC inatarajiwa kuondoka nchini Jumatano kwenda Mauritius kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Cercle de Joachim uliopangwa kuanza Saa 9:30 Alasiri kwa saa za huko Uwanja wa Curepipe mjini Curepipe.
Na timu hizo zitarudiana wiki mbili baadaye, Februari 27 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Lakini mara tu baada ya mchezo wa kwanza na Joachim nchini Maurtius, Yanga itarejea kwenye Ligi Kuu kwa ajili ya mchezo na mahasimu wa jadi, Simba SC Februari 20, mwaka huu Uwanja wa Taifa.
Pamoja na hayo, Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea mwishoni mwa wiki, Stand United wakiikaribisha Simba SC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Mgambo JKT na African Sports Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Mbeya City na Toto Africans Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Ndanda FC na Majimaji Uwanja wa Nangwanda SIjaona, Mtwara na JKT Ruvu na Kagera Sugar Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Februari 14 kutakuwa na mechi mbili, Mwadui FC dhidi ya Prisons Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga na Coastal Union na Azam FC Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Chapisha Maoni