Kwa mujibu wa Ripoti toka Gazeti la The Citizen, Klabu ya Simba tayari imeshalipwa Shilingi Milioni 600 zikiwa ni Ada ya Uhamisho ya Mchezaji wao Emmanuel Okwi kwenda Etolie du Sahel ya Tunisia kama ilivyoamriwa na FIFA.
Simba ilimuuza Okwi, Mchezaji kutoka Uganda, kwa Klabu hiyo ya Tunisia Januari 2013 lakini imekuwa ikipigwa chenga kulipwa Fedha zao hadi ilipotoka Amri hiyo ya FIFA iliyoitaka Etoile kulipa Dola 300,000 pamoja na Faini ya Dola 2,000 la sivyo itapewa Adhabu kali ikiwemo kushushwa Daraja.
Kwa mujibu wa The Citizen, chanzo toka ndani ya TFF kimedai Simba ililipwa Fedha hizo kama Siku 10 zilizopita ikiwa ni kabla ya mwisho wa Siku 90 ambazo zilipaswa kwisha Machi 5.
Gazeti la Citizen pia limedai Msemaji wa Simba, Haji Manara, amesema wao hawajapata Fedha zao toka Etoile ingawa wapo kwenye mchakato wa kuzipata.
Nae Rais wa Simba, Evans Aveva, alikataa kuzungumza lolote kuhusu Malipo hayo aliphojiwa na The Citizen kuhusu Malipo ya Okwi.
Baada ya Simba kumuuza Okwi kwa Etoile Mchezaji huyo hakudumu huko baada ya kutokea mvutano mkubwa kati yake na Klabu uliomfanya arudi kwao Uganda na kujiunga na SC Villa na kisha akajiunga na Yanga na baadae kurudi tena Simba.
Agosti 2015, Simba ilimuuza tena Okwi na safari hii akaenda Klabu ya Denmark, Sonderjyske ambako amesaini Mkataba wa Miaka Mitano.
Chapisha Maoni