Liga yaani Barcelona na Real Madrid. Mchezo huu maarufu kwa jina la El-Classico wenye kubeba hisia ya aina yake na pengine unaoangaliwa na watu wengi zaidi ulimwenguni utapigwa kunako dimba la Nou Camp majira ya saa tatu na nusu kwa saa za Afrika Mashariki.
Mchezo huu unaonekana kunoga zaidi kutokana na vigogo hawa wawili wa La Liga kufundishwa na makocha ambao pia walishawahi kuzichezea timu hizo na kukutana katika El Classico za wakati huo. Barcelona ikifundishwa na Luis Enrique huku Real Madrid ikiwa chini ya Zinedine Yazid Zidane ‘Zizzou’
Wakiwa na rekodi nzuri kabisa msimu huu, Barcelona kwa sasa wamecheza michezo 39 katika michuano yote bila ya kufungwa, mara ya mwisho kupata kipigo ilikuwa ni dhidi ya Sevilla ambapo walikubali kipigo cha mabao 2-1 Oktoba mwaka jana, wakiwa wamecheza michezo 39 mpaka sasa, wameshinda 30 huku michezo 9 wakitoa sare.
Real Madrid kwa upande wao, watakuwa wakitafuta namna ya kupunguza kasi ya Barcelona kutokana na kuachwa nyuma kwa pointi kumi. Ikumbukwe tu kwenye mchezo wa awali uliochezwa kunako dimba la Santiago Bernabeu, Madrid wakiwa chini ya Rafa Benitez wakati huo walikubali kipigo cha mabao 4-0.
Zidane kwa mara ya kwanza kabisa anaingia katika mchezo huu wa El Classico akiwa kama kocha.
Takwimu muhimu za mchezo
Mpaka sasa Barcelona wamecheza michezo 39 bila ya kufungwa, wakishinda 30 ndani ya michezo yao ya mwisho 39, huku michezo miwili tu wakiwa wametoa sare.
Huu ni mchezo wa nne wa El Classico kwa kocha wa Barcelona Luis Enrique akishinda mitatu na kupoteza mmoja ambapo alifungwa magoli 3-1 katika dimba la Santiago Bernabeu
Barcelona wametoka sare mchezo mmoja tu wa ligi kati ya 15 waliyocheza nyumbani, na kushinda yote iliyosalia
Kati ya magoli ya ligi 86 waliyofunga Barcelona, 54 wamefunga wakiwa maskani kwao Camp Nou, huku magoli 23 kati ya 54 yakifungwa katika michezo yao 5 ya mwisho waliyocheza nyumbani
Real Madrid kwa sasa wameshinda mechi zao tano mfululizo
Huu ni mchezo wa kwanza kabisa wa El- Classico kwa Zidane aiwa kama kocha
Real Madrid wamefunga magoli mengi zaidi katika ligi kuliko timu yoyote msimu huu. Wamefunga magoli 87 katika michezo 30 mpaka sasa
Mara ya mwisho Real Madrid kushinda katika uwanja wa Camp Nou ilikuwa ni mwaka 2012, ambapo waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Taarifa muhimu za timu:
Barcelona
Jeremy Mattieu atakosekana kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya misuli aliyopata wakati akiwa timu ya taifa.
Andre Inesta ataanza huku Mturuki Arda Turan akianzia kwenye benchi, Sergio Busquet kama kawaida atakuwa katikati kutuliza mashambulizi ya Real Madrid wakati Sergi Roberto pia akianzia benchi.
Jordi Alba kuna uwezekano akakosekana kama daktari atathibisha bado hayuko fiti, hivyo Aleix Vidal anaweza kuanza.
Mfumo wanaotarajia kuutumia Barcelona: (4-3-3)
Ter Stegen, Alves, Alva, Mascherano, Pique, Rakitic, Busquets, Iniesta, Messi, Suarez, Neymar.
Real Madrid
Sergio Ramos na Bale wanasumbuliwa na majeraha madogo lakini upo uwezekano wakaanza endapo ripoti ya daktari itathibitishwa wako fiti.
Karim Benzema kama kawaida yake atakuwa mbele kuongoza mashambuliz akisaidiana na Cristiano Ronaldo.
Wanaotarajia kuanza kwa upande wa Real Madrid: (4-3-3)
Navas,Marcelo, Pepe, Ramos, Carvajal,Kroos, Casemiro, Modric, Bale, Benzema, Ronaldo.
Barcelona Vs Real Madrid: Takwimu za michezo ya nyuma waliyokutana (head to head)
Tangu kuingia kwa karne ya 21, zaidi ya El-Classico 35 zimechezwa. Hata hivyo kwa kuangalia tu mapambano kumi ya mwisho.
Katika michezo kumi ya mwisho ya El-Classico, zote kwa pamoja Real Madrid na Barcelona zimeshinda mara nne huku michezo miwili iliyosalia ikiisha kwa sare.
* Kwa kuongezea tu, hakuna El-classico yoyote tangu mwaka 2000 ambayo imemalizika bila ya timu hizo kufungana magoli, huku ndani ya mipambano 36 waliyokutana wakiwa na wastani wa kufunga goli moja ndani ya dakika 90.
Asante kwa kutembelea Hope FM Iringa, Asante kwaku-share habari hii, Kama una Maoni, Ushauri, Story ya ku-share na sisi na au Unahitaji msaada...!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni