Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Manchester City watakutana na Real Madrid kwenye Nusu Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI baada ya kufanyika Droo ya kupanga Mechi hizo hii Leo huko Nyon, Uswisi.
Nusu Fainali nyingine ni kati ya Bayern Munich na Atletico Madrid.
Mechi za Kwanza za Nusu Fainali zitachezwa Aprili 26 na 27 na Marudiano ni Mei 3 na 4 huku Fainali ikichezwa huko Mjini Milan, Nchini Italy kwenye Uwanja wa San Siro hapo Mei 28.
Droo hii ya Leo inamaanisha Straika wa Real Cristiano Ronaldo, ambae ndie Mfungaji Bora wa Mashindano haya akiwa na Bao 16, anarejea Jijini Manchester ambako aliwahi kuchezea Mahasimu wa Man City, Manchester United.
Ronaldo, mwenye Miaka 31, pia ndie anaongoza katika Ufungaji Bora wa Mashindano haya katika Historia akiwa na Bao 93 katika Mechi 125.

DONDOO MUHIMU
-Timu zilizotinga Nusu Fainali:
Atlético Madrid (ESP)
Nusu Fainali ya mwisho kucheza:
2013/14 (Walishinda 3-1 v Chelsea)
Rekodi yao Nusu Fainali: W2 L2
Rekodi yao Msimu huu: W5 D3 L2 F14 A5
Mfungaji Bora: Antoine Griezmann 6
Uso kwa Uso na Timu nyingine za Nusu Fainali:
v Bayern W0 D1 L1 F1 A5
v Manchester City Hawajakutana
v Real Madrid W1 D1 L4 F4 A9
Bayern München (GER)
Nusu Fainali ya mwisho kucheza:
2014/15 (Walifungwa3-5 v Barcelona)
Rekodi yao Nusu Fainali: W10 L7
Rekodi yao Msimu huu: W7 D2 L1 F28 A9
Mfungaji Bora: Robert Lewandowski 8
Uso kwa Uso na Timu nyingine za Nusu Fainali:
v Atlético W1 D1 L0 F5 A1
v Manchester City W3 D0 L3 F9 A8
v Real Madrid W11 D2 L9 F33 A31
Manchester City (ENG)
Nusu Fainali ya mwisho kucheza:
Nusu Fainali ya kwanza kabisa kwao
Rekodi yao Nusu Fainali: W0 L0
Rekodi yao Msimu huu: W6 D2 L2 F18 A11
Mfungaji Bora: Kevin De Bruyne/Raheem Sterling 3
Uso kwa Uso na Timu nyingine za Nusu Fainali:
v Atlético Hawajakutana
v Bayern W3 D0 L3 F8 A9
v Real Madrid W0 D1 L1 F3 A4
Real Madrid (ESP)
Nusu Fainali ya mwisho kucheza:
2014/15 (Walifungwa 2-3 v Juventus)
Rekodi yao Nusu Fainali: W13 L13
Rekodi yao Msimu huu: W8 D1 L1 F26 A5
Mfungaji Bora: Cristiano Ronaldo 16
Uso kwa Uso na Timu nyingine za Nusu Fainali:
v Atlético W4 D1 L1 F9 A4
v Bayern W9 D2 L11 F31 A33
v Manchester City W1 D1 L0 F4 A3
**W=Walizoshinda D=Sare L=Kufungwa F=Magoli ya Kufunga A=Magoli ya Kufungwa

TAREHE MUHIMU:
-Droo ya Nusu Fainali: Aprili 15
Mechi Aprili 26/27 na Marudiano Mei 3/4
FAINALI
Mei 28
San Siro, Milan, Italy



Chapisha Maoni