Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




Na Alex Mapunda
 Rashid  Idd chama.

“kabla ya kwenda  kushiriki michuano ya kombe la mataifa  ya Afrika  mwaka 1980 nchini Nigeria tulienda kuweka kambi ya mwenzi mmoja nchini mexico  na tulicheza mechi za kirafiki hili kujiweka fiti kukumbana na wapinzani wetu nchini Nigeria.

Nakumbuka  kuna mchezo tulienda kucheza  katika mji wa starehe ambao upo inje kidogo ya mji mkuu wa mexico,mchezo hule ilikuwa balaa mwamuzi wa mchezo ule aliwatoa wachezaji wetu watatu kwa kadi nyekundu na tayari wapinzani wetu walikuwa mbele kwa bao 2-1,lakini Peter  Tino alifanya kazi zuri na akasawazisha lile bao, ubao ukasomeka 2-2.

Baada ya mchezo ule tulianza kucheza rafu mbaya sana kwa wapinzani wetu kwa kuwa sheria za soka zinasema mwamuzi aruhusiwi kutoa kadi nyekundu zaidi ya  ya tatu uwanjani isipokuwa anaruhusiwa kuvunja mechi,sisi kwa upande wetu tulikuwa tayari mchezo uvunjike  lakini sio kufungwa,tuliendelea kuwapiga buti hadi mwisho wa mchezo  wachezaji wa mexico walitupa heshima na walishukuru mungu mpira kuisha bila kuvunjika mtu”.

Sio mwingine ni Rashidi idd Chama kwa wapenda mpira  watamkumbuka milele kutokana na uwezo wake  mkubwa wa kusakata kandanda ambao alikuwa nao  hasa miaka ya 1976 hadi miaka ya 1990 akiwa na klabu mbali mbali pamoja na  timu ya taifa .

Chama mzaliwa wa Tabora eneo la ng’ambo, alianza kusakata kandanda akiwa katika shule ya msingi miembeni kisha Sekondari  ya kinondoni zote za Jijini Dar es salam  nyota yake ilianza kung’ara toka  mwaka 1971 wakati alipukuwa akitumikia kikosi cha watoto  katika timu ya yanga kwa kipindi cha miaka 5 ambapo mwaka 1976 alisajiliwa rasmi kuchezea  timu ya wakubwa  ya Dar es salam yang   Africa,kutokana na umahili wake mkubwa wa kucheza namba zote katika safu ya ulinzi alipata nafsi hiyo akiwa na umri ya miaka 17 ambapo bado ailikuwa hajaitimu elimu ya shule ya msingi[darasa la 6].


Mwaka 1977 Chama alichaguliwa kuchezea timu ya taifa ya vijana mara baada ya jopo la makocha wa timu ya taifa  kubaini uwezo wake na mwaka mmoja baadae akachaguliwa kutumikia timu ya wakubwa ‘Taifa Stars’ ambapo kwa mara ya kwanza  walienda kushiriki michuano ya  challenge mjini Nairobi.

Na katika michuano hiyo timu ya taifa ya Tanzania ilitolewaa  na timu ya Taifa ya Malawi katika mchezo wa nusu fainali kwa stahili ambayo  haijatokea   tena  katika soka,mchezo kati ya Tanzania na Malawi ulichezwa siku tatu,siku ya kwanza  timu zote zilitoka sare ya bila kufungana  zikapigwa penalti 5 kwa kila upande  ambapo timu zote zilipata ushindi katika penalti hizo mchezo ukahailishwa adi siku ya pili kwa kuwa sheria za kipindi kile  zilikuwa  haziruhusu mapigo ya ziada ya penalti baada ya penalty tano kupigwa.

Timu zote mbili zikalazimika kuingia uwanjani siku ya pili ili kujaribu tena bahati zao lakini kwa mara nyingine mchezo ulimalizika kwa sare ya penalti 5-5 hali ambayo ilipelekea mchezo huo kusogezwa hadi siku ya Tatu huku hali ya kukamiana kwa timu hizo ikaongezeka mara dufu,lakini siku ya tatu jahazi la Tanzania lilienda mlama mara baada ya  mchezaji wa Tanzania kasimu manara, kukosa penalty baada ya  timu hizo  kutoshana nguvu kwa mara nyingine ndani ya dakika 90 ambapo Malawi walipata nafsi ya kuingia fainali huku  Killi Stars wakakumbana na ndugu zao toka visiwani Zanzibar  katika kinyang’anjiro cha kumtafuta mshindi wa tatu na wakafainikiwa kuichabanga bao 2-0 zikisukumizwa wavuni na Peter  Tino.

Mwaka 1979 chama aliwapa kisogo yanga na akatimukia Pan  Afrika timu ambayo aliitumikia adi mwaka 1982 na akarudi tena Jangwani baada ya kuikosa timu hiyo kwa muda mrefu ambapo alicheza yanga adi mwaka 1988 alipoamua kujiunga na  Maji Maji ya Songea timu ambayo aliichezea kwa misimu kadhaa  ambapo mwaka 1990 aliitajika na klabu ya Pamba toka mkoani mwanza.

Safari yake ya mwanza iliambatana na mikosi kwa kuwa  kabla ya kucheza mechi yeyote ya ligi timu ya pamba ilienda nchini Burundi kucheza michezo yz mjaribio kabla ya ligi kuaza  kitu ambacho kilimkumba aliumia mguu pasipo kucheza mchezo wowote  na akafungwa pio pii na ndoto za kuchezea pamba zikagonga ukuta akaamua kurudi Dar.

Baadae mwaka 1991 katibu ya kampuni ya ndovu  bwana Twaa funguo alimchua toka dar ili kuchezea timu ya kampuni hiyo timu ambayo  aliichezea adi mwaka 1996 hapo ndipo  aka kaa chini ya mti na kusema imetosha sasa,akaachana na soka,anaeleza Iddi chama  kwa umakini kasha anaendelea;-

Watu walinifitini Ndovu.

“Wakati niliposajiliwa ndovu mwaka 1991 watu wengi walinifanyia fitina kwa  wivu wao  ambao haukuwa wa msingi huku wakidai kuwa uwezo wangu wa kusakata kandanda ulikuwa ukingoni lakini sikujali maneno yao,kitu ambacho nilikifanya ni kuhakikisha natimiza yale yote ambayo yalinipeleka ndovu na hatimaye walikuja kuikubari kazi yangu ya uwanjani.

Amecheza mashindo yote ya vilabu na timu zote  za taifa Africa.

“Nimecheza klabu bingwa afrika,kombe la Shirikisho kipindi kile kombe la washindi,michuano inayoandaliwa na nchi za ukanda wa Afrika mashariki na ngazi ya vilabu na timu ya Taifa lakini kubwa zaidi kushiriki michuano ya mataifa huru ya afrika michuano ambayo kwa Tanzania ilikuwa ni mara ya kwanza na mwisho kwa kuwa adi dakika hii ile rekodi bado haijavunjwa tena kwangu mimi najisikia faraja kubwa sana.

“Sisi wachezaji wa miaka ya 1970 sijisifii tulikuwa na uwezo wa hali ya juu sana kuanzia  mazoezi na uwezo wa kusakata kandanda ambao mwenyezi mungu alitujalia na kikubwa lila mchezaji alikuwa makini na wachezaji wengi wa kipindi kile waliupenda mpira kwa dhati tofauti na wachezaji wa zama hizi.

kombe la mataifa ya afrika 1980,mwanaume ndani .

“mimi niliuwa ni miongoni mwa wachezaji wachache ambao tulibahatika kwenda kuwakirisha taifa letu  nchini Nigeria ingwa nilikuwa na umri mdogo sana  kuchezea timu ya Taifa kwa kuwa niliwanyang’anya namba watu ambao nilikuwa nawaeshimu sana katika soka la hapa nchini,kiukweli nilifarikika sana.

“kutokana na ushindani ambao ulikuwepo kwa wachezaji hadi dakika za mwisho wachezaji ambao walikuwa na uhakika wa kwenda Nigeria walikuwa ni wawili pekee ambaye ni Juma ponda mali pamoja Athumani mambosasa kwa kuwa walikosa upinzani kwa upande wa magolikipa  hapa nchini, walikuwa wanatisha.

“baadhi ya wachezaji ambao  tulipata nafasi adimu ya kwenda  Nigeria  kupeperusha bendela ya nchi yetu ni pamoja na Juma pondamali,Athumani mambo sasa,Reopard Mkebezi, pamoja na Mohamed Kajore [marehemu]

“wengine ni Redga Tenga,Jela mkagwa,Juma mkambi [marehemu],Omari husein,bila kumsahau Husain Ngurungu,pia wakichagizwa na  mimi mwenyewe,Mohamed salumu,Piter Tino  pamoja na mtu mzima  Ally,tuli kuwa wengi hao ni baadhi ya ninaowakumbuka.

“Tukiwa inchini Nigeri huku tukiwa na presha kubwa ya mashindano mchezo wa kwanza tulipepetana na wenyeji Nigeria tulichezea kichapo cha bao 2-1,sawa na matokea ya mchezo ambao ulifuata  ambapo pia waarabu toka Misri yalitufumua bao 2-1,ambapo tulijikongoja katika mchezo ya mwisho dhidi ya Tembo wa afrika Ivory Coast kwa matokeo ya sare ya bila kufungana.

Kikubwa ambacho  kilituponza kutolewa mapema ilikuwa ni woga wa mashindano kwa kuwa ili kuwa mara yetu ya kwanza  kushriki fainali za mataifa ya afrika, kwa upande wa uwezo wa kusakata kandanda kwa asilimia kubwa tuliwazidi  na  kinachoniumiza mara baada ya kutolewa katika michuano ile hadi leo hii hatujapata tena nafsi ya kushiriki mashindano makubwa kama yale kila nikikumbuka roho inauma sana.

Imani za kishirikina

“siweze  kukataa hayo mambo yapo sana watu kuvaa irizi uwanjani pamoja na kuchinja  mbuzi kwa hizi timu zetu kubwa  haya mambo yapo sana,lakini mimi baba yangu alinipa wosia kwamba mara zote katika shughuli zangu zote nimtangulize mwenyezi mungu  yeye ndiye mwenza wa yote,na katika mpira silaha pekee ni mazoezi na  kipaji cha kuzaliwa nacho vinginevyo hata kama ni mtoto waganga mpira utakushinda.

Soka la sasa na zamani.
“vijana wetu wa sasa hawajitambui starehe  zimezidi tofauti na enzi zetu tulikuwa  na nidhamu ya hali ya juu ndio maana tulikuwa na miili ya kucheza mpira, kiukweli mpira na starehe ni vitu ambavyo havitangamani lanzima wachezaji wetu wa sasa wabadilike.

Anaowapenda.
“ Agrey Moris,kelvin yondani,Aathumani Idd pamoja na mchezaji chipukizi wa wekundu wa msimbazi Ramadhani Singano [MESSI] wanajitaidi kucheza vizuri,

 Ushauri kwa soka la Tanzania.

“Rais washirikisho la mpira wa miguu hapa nchini awatambue  na kueshimu  mchango wa wachezaji wa zamani ambao utakuwa msaada mkubwa kwa timu yetu ya taifa ,kama atapuuzia wazo hilo bado vijana wetu watakosa madini toka kwa wakongwe.

“sisi wachezaji wa zamani hapa nchini kusema kweli hatutambuliki kama wachezaji wezetu wanavyotambulika kwenye nchi nyingine,viongozi wa sasa wasiteue viongozi wa soka kisiasa toka katika ngazi za wilaya lanzima kila mtu awe tayari kubadilisha soka letu.


Baada ya kutundika daruga.

“umri wangu ni miaka 56,nafanya biashara ndogo ndogo pia nina duka la vifaa vya michezo hapa mjini Arusha,nina mke na watoto  watatu mmoja wakiume ambaye  naamini atarithi mikoba yangu  pia yupo kwenye kituo cha michezo ambacho nafundisha hapa Arusha nikiwa kama kocha, alikuwepo kwenye michuano ya copa cocacola anaitwa Ibrahim Chama anacheza nafasi ya ushambuliaji.


Chapisha Maoni