Na Alex
mapunda
25-03-2014
Maji maji
FC.
Miongoni
mwa Timu ambazo zilitokea kuwa tishio hapa nchini miaka ya 1980 hadi 2000
ukiziweka kando Simba na Yanga utakubariana na mimi kuwa Maji Maji ya
Songea Maarufu kwa Jina la Wanalizombe ilikuwa tishio hapa nchini.
Maji Maji
ambayo Ilizaliwa rasmi mwaka 1977 kwa muunganiko wa timu mbali mbali mjini
Songea chini ya Mwasisi wa timu hiyo Dk Roulence Gama ilianza kupata umaarufu
mkubwa mwaka 1980 mwaka ambao timu hiyo ilipata nafasi ya kushiriki kwa mara ya
kwanza ligi Daraja la kwanza hapa nchini.
Licha ya
kuwa na uwezo mzuri uwanjani na kusajii wachezaji wazuri Maji Maji haikubaki
nyuma kwa kuamini Imani za kishirikina,imani ambazo zimetayala soka la Tanzania
tangia miaka ya nyuma,Jelamba Viwanjani
baada ya kufanya utafiti wa kina imefanikiwa kunasa baadhi ya matukio ya
kishirikina ambayo yametokea katika klabu hiyo kupitia kwa wachezaji na
viongozi ambao wamewai kutumikia timu hiyo katika nyakati tofauti, kama
wanavyofafanua ;-
ALLY
MCHUMILA
Wakati natumikia Maji Maji kama Meneja mchezaji nakumbuka Tulimsajili
Mzee wa kamati ya ufundi nje ya uwanja toka Afrikan Sports Mzee ambaye
alikuwa na uwezo wakusimulia matukio yote ya uwanjani wiki moja kabla ya mchezo
na wao aliwapa ubingwa,ambapo baada ya kumsajili tulienda kucheza na
Yanga Jijini Dar es salam mchezo ambao ilikuwa mgumu sana kwetu lakini
Yule mzee wiki moja kabla alituambia kuwa Yanga Tutawafunga Bao
1-0,bao ambalo litafungwa na beki sio mshambuliaji.
Kweli mchezo ulikuwa mgumu sana kwa pande zote lakini mimi na viongozi wenzangu
tulijiamimi sana kwa kuwa mtaalaum Alisha tuambia matokeo ya mchezo, ambapo
kama alivyosema Yule Mzee beki wa Maji Maji Piter Mhina aliwafunga midomo
mashabiki wa yanga kwa kufunga bao safi ambalo lilidumu hadi dakika
90 za mchezo zipomalizika.
SHAIBU
KAMBANGA
''Mwaka
1996 mzee wa timu ya Maji Maji sitamtaja jina kwa kuwa namweshimu sana alituita
chumbani na kutufunika shuka nyeupe akaanza kupiga Manyanga mimi nilikuwa
nimekaa na marehemu Kisochi lemba mzee alikuwa anaongea lugha ambayo hakuna
aliyekuwa anaielewa lakini ilikuwa kila akipita nilipo mimi nilisika neno la
mwisho akisema Maji Maji tufungwe tatu na Simba nilijaribu kumweleza mwezamu
yeye akasema sio kweli ila mzee kasema Maji Maji tushinde tatu,niliendelea
kumsikiliza yule mzee kwa makini sana na baada ya tukio lile nilijalimu
kuwaeleza wenzangu wote walishangaa.
''Tukaja
kwenye mechi mchezo ulikuwa mgumu sana upande wetu na kama yule mzee nilivyomsikia
mimi Simba walitubugiza bao 3-0
KENNETH
WANE
“Tukio
hili hadi naingia kaburini siwezi kusahau,nakumbuka mwaka 1995 tulienda mwanza
kucheza na Pamba ya mwanza viongozi wa Maji Maji wakatupeleka kwa mganga
wa Toto Afrika ili kutufanyia dawa kwa kuwa toto na pamba walikuwa
wapinzani wakubwa.
“Siku
hiyo tulichanjiwa dawa na kila mmoja aliogeswa dawa Ndoo mbili na tulipelekwa
wachezaji 7,lakini mimi sikufurahishwa na kitendo cha kuchanjwa dawa nikamua
kumdanganya mganga ili asinichanje nilichokifanya nikamwita pembeni na
kumwambia kuwa wakati nipo mdogo nilipatwa na ugonjwa wa ajabu na wazazi wangu
wakanipeleka nchini msumbiji ili kunifanyia dawa ambapo mganga wa msumbiji
alinichanjia dawa na akaniambia mtu yeyote arusiwi kunichanjia dawa hadi kitoke
kibari toka kwake baada ya kumweleza hayo mganga akaduwaa!
“ baadae
akanipa ilizi ambayo niliiweka kwenye ugoko ,pia baada ya kuoga dawa mganga
alituagiza tukatafute kuku na kumchinja saa saba usiku na damu yake
kuchanganywa na maji pia kuoga kitu ambacho tulikitekeleza,lakini baada ya
Dakika 90 za mwamuzi kukamirika pamba 5-1,ali ambayo ilitufanya tutoke uwanjani
vichwa chini.
ISIHAKA
MAJALIWA
Mwaka
1983 kulikuwepo na mechi kali sana kati yetu na Simba toka jijini Dar es salam
mechi hile ilichezwa wakati kamati ya ufundi ya Simba ilikuwa inaongozwa na
kikosi ambacho kilikuwa imesheni vichwa toka Brazil na wakati tunakutana nao
Simba ilikuwa imezindua mfumo mpya wa kibrazili maarufu Kama ‘Kanivo Samba’
hakika simba ile ilikuwa inatisha.
“Nikiwa
kipa namba 1 wa timu yetu Viongozi wakanichukua na kunipeleka kwa
Mganga wa jadi ambaye sasa ni Marehemu ili kuchukua mbinu za kuidhibiti Simba.
“Wakati
wa asubuhi nakumbuka mganga aliniambia kuwa, mechi itakuwa ngumu sana
kutokana na uimala wa wapizani wetu,usiku wa leo nimejitaidi kuokoa magoli
mengi sana kadili ya uwezo wangu lakini hata hivyo yamebakia magoli mawili
ambayo nitayamalizia uwanjani wakati mechi ikiendelea.
“Wakati
wa mchezo ulipowadia timu zote zikaingia uwanjani na mechi ikaanza,mechi
ilikuwa ngumu sana na Simba walipata bao 2 za wazi lakini waamzi wa mchezo ule akayakataa
na kusema wafungaji waliotea[off side] na hadi mwisho wa mchezo
tukatoshana nguvu ya bila kufungana,hapo ndipo nikakumbuka maneno ya mganga na
kuamini uwezo wake.
JOHN
KABISAMA
“Mwaka
1985 kulikuwa na pambano kali kati ya maji maji na Pan Afrika pambano ambalo
ilitakiwa lichezwe siku ya Jumamosi lakini pan walichelewa kufika uwanjani kwa
sababu ambazo hazikuwekwa wazi na pambano likahailishwa adi siku ya Jumatatu.
“Kipindi
hicho Maji Maji alikuwa imemuleta mzee wa kamati ya ufundi Toka Kigoma ambaye
alikuwa anahakikisha kamati ya ufundi nje ya uwanja inakwenda sawa.
“Yule
Mzee tulimpa jina la Mzee Mziba jina la mchezaji maarufu kutokea kigoma,kwa
kweli mimi nilikuwa siamini imani hizo lakini yule mzee nilimweshimu
sana,nakumbuka alituambia kuwa mechi yetu na Pan itachezwa siku ya
Jumatatu tutashinda bao 3-0,na hata kama tukipata nafasi nyingine ya kufunga
bao haitawezekana.
“kwa kipindi kile Pan Afrika likikuwa Tishio
Mimi sikuafiki kama tungeweza kupata ushindi mkubwa kiasi kile lakini sisi
tulikuja kuamini mara baada ya kumalizika ule mpambano ambapo tulishinda bao
3-0 kama alivyotuambia yule mzee,hali ambayo ilinishanganza sana.
Pia
yule mzee mwaka 1985 alitabili mchezo wetu dhidi ya simba kuwa tungeshinda bao
2-1 kitu ambacho kweli kilitokea ambapo yule mzee alituwezesha maji maji
kuchukuanubingwa mwaka 1985 kutokana na ubora wa dawa zake.
GOD
MVULA.
“Baba
yangu alikuwa mkurugezi wa Matimila Bendi pia ilikuwa karibu sana na Mzee gama
kipindi hicho nipo shule ya msingi kulikuwa na wimbo ambao
ilitungwa na Amza Clara chini ya bendi yake,wimbo ambao ulifahamika kwa jina la
mchaka Mchaka.
“Wimbo wa
mchaka mchaka uliusishwa na imani za kishirikina ulikuwa ukipigwa lazima lazima
Maji Maji Ipate ushindi pia ilichochea Morali kubwa kwa timu ya Maji Maji na
ikapelekea kupata umaarufu mkubwa.
Kwa
matukio hayo machache licha ya Maji maji ya hivi sasa kukumbwa na tatizo la uchumi
tatizo ambalo linaelezwa ni chanzo kikuu cha timu hiyo kufanya vibaya kuazia
mwaka 2000 hadi hii leo pia unaweza kukubariana na mimi kuwa kamati ya ufundi
ya kuimalisha timu hiyo imekosa wataalam kama akina mzee mziba ambao waliifanya
kazi hiyo kwa kiwango cha hali ya juu sana.
Ujenzi
wa Maji maji mpya.
Pia
maji maji ya sasa ili iweze kurudisha makali yake ya zamani lazima wanaruvuma
wote waweke shida zao chini na kurusha mikono juu, huku wakisahau tofauti zao
pasipo kujali itikadi,dini,ukabira,siasa na hata jinsia kinyume na hapa maji
maji itaendelea kubaki kichwa cha mwenda wazimu,huku wakimsaka mchawi wa timu
hiyo wakati wachawi ni wenyewe.
Chapisha Maoni