Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


 TAREHE 29-03-2014

 FIFA World Cup 2014 - Finals Tickets

 Kombe la dunia ni michuano ambayo imepata umaarufu mkubwa duniani kwa kutanzamwa na watu wa rika zote wakiwemo akinamama,akinababa,vijana na pia watoto wadogo  na katika kipindi chote ambacho kombe hilo limechezwa wakulima maarufu wa zao la kahawa duniani nazungumzia Blazil wametwaa kombe hilo mara tano kuliko nchi yeyote duniani,wakifuatia wataliano ambao wamechukua mara 4.

 kombe hilo lilianzishwa mwaka 1930 ni takribani miaka 12 mbele baada ya kumalizika kwa vita vya kwanza vya dunia mwaka 1918 na michuano hii ilifanyika katika nchi ya Uruguay kuanzia tarehe 13-30 julai.

Mataifa 13, 7 toka Amerika kusini, 4 toka ulaya na 2 toka America kaskazini yalishiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza,ambapo baadhi ya mataifa hayakushiriki kutokana na ugumu wa usafiri kuelekea nchini Uruguay.
Hakukua na mashindano ya awali kupata nafasi ya kushiriki, nchi zote zilizokua chini ya FIFA zilialikwa kushiriki na Zilipewa muda mpaka tarehe 28 mwezi wa pili 1930 kuthibitisha ushiriki wao. Argentina, Brazil, Bolivia, Chile, Mexico, Paraguay, USA, Peru, Belgium, France, Romania na Yugoslavia zilithibitisha ushiriki akiwemo Uruguay.
Nchi hizo ziligawanywa katika makundi manne, na mshindi wa kila kundi alisonga mbele kwa ajili ya nusu fainali ambapo Jumla ya michezo 18 pekee ilichezwa,huku yote ilichezwa katika mji mmoja, Montevideo na viwanja ambavyo vilitumika ni Estadio Centenario, Estadio Pacitos na Estadio Parque Central.

.ambapo katika fainali hizo nchi ya urguay iliandika historia ya kuchua kumbe la dunia kwa mara ya kwanza akiwa kama mwandaaji.

Mwaka huu michuano hiyo inafanyika nchini blazil baada ya afrika kusini kuandaa michuano hiyo mwaka 2010 michuano ambayo ilifanyika katika ardhi ya afrika kwa mara ya kwanza ambapo Hispania alitwaa ubingwa wa michuano hiyo.

Licha ya brazil kuwekwa katika orodha ya moja ya timu ambazo zinapewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo nchini hiyo haijtwaa taji la kombe la dunia katika ardhi yake ya nyumbani,licha ya kuandaa michuano hiyo mwa 1950 ambapo urguay aliibuka kidedea,hali ambayo inaonesha ofu kwa blazil kuwa inaweza ikapoteza kombe hilo kwa mara ya pili katika uwanja wake wa nyumbani licha ya kuwa kinara kwa kuchukua kombe hilo mara Tano lakini katika viwanja vya ugenini.

Kitu cha kuzingatia zaidi katika michuano hii kwetu sisi watanzania ni kuhakikisha tunajifunza kupitia kwa wenzetu ambapo wataenda kutuwakilisha nchini blazil ikiwa ni Takribani miezi miwili imepaki kabla ya kipenga kupurizwa kuashiria kuanza kwa vita ya mataifa 32 toka kila kona nchini blazil,huku watanzania tukiwa hatujawai kufanya vizuri hata katika hatua za mwanzo..


MAKUNDI, RATIBA KUMBE YA KOMBE LA DUNIA.







Chapisha Maoni