TAREHE 28-03-2014-13:41
LIGI kuu ya Vodacom Tanzania maarufu kama VPL imeendelea
kushika kasi huku timu mbali mbali
zikiendelea kuchuana vilivyo ili jujihakikishia zinapata nafsi za kuwakisha
nchi katika michuano ya kimataifa msimu ujao huku zingine zikipigana vilivyo
ili zisikumbwe na mkasi wa kushuka daraja adi ligi daraja la kwanza,hakika
mvutano ni mkubwa sana.
Katika kinyanganyiro cha kuchukua ubingwa timu ambazo
zimeingia katika vita hiyo ni Azam Fc pamoja na timu ya Yanga timu ambazo zimeonekana
kukamiana vilivyo kwa kuwa kila timu inaitaji pointi tatu muhimu ili
kujihakikishia nafasi zuri ya kuchukua ubingwa ambapo takwimu zinaonyesha kuwa
kila timu ina nafasi ya kunyakua ubingwa katika ligi hiyo.
Wanalamba lamba azam Fc wanapewa nafsi kutokana kuongoza
ligi hiyo kwa tofauti ya poinnti 4 huku ikiwa imecheza mechi 22 mkononi ingawa
moja ya mechi ambazo zimesalia ni mechi ambazo zinaelezwa kuwa ngumu kwa kuwa
moja ya mechi hizo ni dhidi ya Simba,kagera sugar pamoja na ile ya
ving’ang’anizi watoto wa Mbeya City.
Mabingwa watetezi wa ligi hiyo wazee wa Jangwani Dar esam Yang Africans wao wanapewa nafsi ya
kutetea ubingwa wao kwa kuwa wamebakiza mechi nyingi ambapo mechi hizo sio
ngumu ikilinganishwa na mechi za wapinzani wao Azam Fc ingawa moja mechi hizo
ni mchezo dhidi ya wapinzani wao wa Jadi wekundu wa msimbazi simba timu
ambayo kwa misimu miwili sasa haijafanya
vinzuri kutokana na migorogo mingi ambayo inafurukuta katika kalabu hiyo,kwa
takwimu hizo kila timu kati ya yanga
pamoja na Azam zote zinanafsi zuri za kufunzu licha ya Mbeya City kuendelea
kunyatia kwa nyuma nayo ikipigania nafsi mbili za juu.
Vile vile ligi kuu ya Vodacom Tanzania kwa msimu huu
tumeshuhudia mabadiliko makubwa baada ya ujio wa kishindo wa mbeya City pamoja
na kuimalika kwa timu ya Costal Union toka mkoani Tanga ali hiyo imesababisha
timu kubwa hapa nchini kama mtibwa Sugar kupoteza nafsi zao kutokana na
uwekezaji mdogo ambao timu hiyo imefanya kwa msimu huu huku baadhi ya wakereketwa wa masuala ya soka
wakidai kuwa benji la ufundi la mtibwa sugar halijajipanga vizuri.
Licha ya yote vita nyingine ambayo kwa upande mwingine kama
TFF wasipokaa sawa inaweza ikatawaliwa na Fitina kubwa ni ile ya kuchuka Daraja
ambapo kila timu inaitaji kubaki ligi kuu hali ambayo inaweza ikasababisha kuwepo kwa
mazingira ya timu kuuza mechi au kununua
mechi hii inachagizwa na udhamini mnono ambao azam Fc wameutoa kwa vilabu vyote
vya ligi kuu kotokana na haki za matangazo.
Timu hizo ambazo zipo katika mstari mwekundu wa kushuka daraja
ni pamoja na wauza mitumba wa Ilala ashati united wenye pointi 18 baada ya
kucheza mechi 22,wafunga buti toka Arusha
JKT oljoro ambao wana pointi 15 baada ya kukiputa mara 22 huku Rhino Rangers wakiendelea kuburuza mkia
katika ligi hiyo kwa kufikisha pointi 13 mara baada ya kucheza mechi 22 hali
ambayo inaashiria kuwa Tayari taa nyekundu imeshawaka kwa wageni hao ambao
walipanda daraja msimu uliopita.
Kwa maana hiyo adi kufikia hivi sasa bado ni kitendawili
kikubwa kujua kati ya yanga au Azam ni nani
kati ya hao atachukua kombe msimu huu, ingawa
Azam Fc inapewa nafsi kubwa ya kuchukua Taji hilo kwa kuwa tayari
inaongoza kwa tofauti ya pointi nne
ambapo amefkisha pointi 47 huku akifuatiwa na yanga yenye pointi 43.
Chapisha Maoni