Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



Na Alex Mapunda,Iringa
 
 Displaying WP_000571.jpg


 MICHUANO ya pool kwa vyuo vikuu hapa iringa
inatarajiwa kufanyika tarehe 12 mwenzi wa nne badala ya mwenzi wa tatu
kama ilivyoelezwa hapo hawali na mwenyekiti wa pool mkoa bwana salum
Kisaku.



 Mashindano hayo ambayo yanatarajia kufanyika kwa mara ya nne safari
hii yatashirikisha vyuo vinne ambavyo ni chuo kikuu iringa,Ruko Mkwawa
pamoja na CDTI na mdhamini wa mishuano hiyo ni kampuni ya bia ya TBL.

''kila kitu kinaenda vizuri ambapo washindi wa michuano hiyo watapewa
zawadi  kama ilivyokuwa kwa miaka mingine na kikubwa tumeamua
kuyasogeza hadi mwenzi wa nne, moja ya sababu ikiwa ni baadhi ya vyuo
vilikuwa na likizo na bila shaka sasa ivi vyuo vyote vimefungua
 na wameanza  kufanya maandalizi ya michuano hiyo,alisema kisaku.


Timu ya chuo cha Ruko wameibuka na ushindi kwa mara zote ambazo
michuano hiyo himefanyika ambapo kwa sasa kila timu inajinoa ili kuhakikisha
inakua ya kwanza kuvunja mwiko wa Ruko kuwa kinara katika mashaindano hayo.

Chapisha Maoni