Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




Azam FC imefanikiwa kuweka rekodi mpya kwa kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya kwanza.

Azam FC imeukosa ubingwa huo mara mbili mfululizo ikishika nafasi ya pili, lakini sasa imemaliza kazi kwa kuifunga Mbeya City kwa mabao 2-1 kwao Sokoine mjini hapa, leo.

Katika mechi hiyo iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu, huku Azam FC ikitaka pointi tatu kumaliza kazi, wageni ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Gaudence Mwaikimba katika dakika ya 45.

Lakini Mbeya City wakasawazisha kupitia Mwagane Yeya katika dakika ya 70 kabla ya nahodha John Bocco kutupia bao la pili na kuhitimisha safari yao ya kutwaa ubingwa wakiwa na mchezo mkononi dhidi ya Ruvu JKT.

Hii ni mara ya kwanza kwa Azam FC kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara huku ikipangua ‘minguvu’ ya wakongwe Yanga na Simba ambao wanabaki katika nafasi ya pili na nne.



Chapisha Maoni