ENDELEA
KUFUTALIA HISTORIA YA STIVIN MAPUNDA GARRINCHA LEO ANASIMULIA TUKIO LA KUFUNGIWA NCHINI NIGERIA,PAMOJA NA KURUDI MAJI MAJI AKITOKEA SIMBA
Kurudi Maji Maji.
STIVINI MAPUNDA GARRINCHA ALIYEVAA TSHETI NYEUSI KULIA.
“mwaka 2005 niliamua kurudi maji maji
kutokana na migogoro ambayo ilikuwepo ndani ya clabu ya Simba hali ambayo
ilipelekea mimi na mwezangu kufungiwa pasipo kujua kosa letu na kututaka
kuandika barua kwa kuwa sikuwai gombana na mtu yeyote ndani ya Simba nikaamua
kuondoka kwa Moyo mweupe na kurudi katika timu yangu ya Zamani Maji Maji
Fc.
“niliendeleza soka nikiwa na maji
maji toka nilipotoka Simba kwa misimu Kadhaa na baadae nikaamua kutundika
daruga na kujishughulisha na shuguli za kawaida.
TULIFUNGIWA SIKU NNE NCHINI NIGERIA
“mwaka 2004 tulifungiwa chumbani
siku 4 nchini Nigeria na ubarozi wa Tanzania ili kutunusuru tusikamatwe mara
baada ya kuchelewa toka nchini Benin ambako tulitoka kucheza kati yetu na timu
ya Taifa ya Benin mechi ambayo tulifungwa goli 4-0,na mara baada ya kufika
Nigeri tulikosa usafiri baada ya kukuta
ndege ambayo tulitakiwa kusafiri nayo imeondoka na kipindi hicho Tayari
visa zetu kusafiria zilikuwa zimekwisha.
“Barozi wa Tanzania inchi Nigeria
SiSiko ilimlazimu kutufungia chumabani huku tukila nyama na kipande kimoja na
mkate mara moja kwa siku kama Gerezani kwa uzembe ambao ilifanywa na viongiozi
wetu,na hatimaye siku ya 4 tulifanikiwa kuondoka na viongozi wetu hawakuwai
kuzungumzia chochote kuhusu tukio lile.
“Inanisikitisha sana kwa timu ya
taifa kukwama ugenini kwa kipindi cha siku 4, mimi binafsi kwa kipindi chote
cha maisha yangu hapa duniani siwezi kusahau”.alisema mapunda.
Endelea kufuatilia
atasimulia ugomvi kati yake na kiongozi wa Fat kipindi kile.
Chapisha Maoni