Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


TAREHE7-04-2014
  Everton FC vs Arsenal FC


Arsene Wenger achape lapa au ambaki? Ndio wimbo unaorindima ndani ya mioyo na midomo ya mashabiki wa Arsenal. Hii ni baada ya kuchapwa 3 na Everton jioni jana. Mashabiki walaumu Wenger naye Wenger wenyewe akilaumu kikosi chake.

"Lililobaki kwa silimia 100 tutang'ang'ania nafasi ya nne ingawaje ni vigumu," Wenger amesema.
Shabiki mmoja auliza katika mtandao wa twitter kuwa iweje January walikuwa nambari moja, february nambari 2, Mwezi wa tatu 3 na sasa mwezi wa nne nambari nne?

Mwingine asema Bwana Wenger amemtetea kwa miaka mingi - tisa kwa idadi -lakini leo amekoma. Amejiunga na wale ambao wameanzisha kampeni katika mtandao Wenger ajiuzulu.

Kilio cha Arsenal ni furaha ya Liverpool ambao baada ya kuitandika West ham 2-1 wametuliza kileleni mwa league - Na bashasha sasa pia zasikika pia katika kambi iliyokuwa imefifia ya Manchester United baada ya kuimwagia machunngu yao yote NEW Castle 4- bila na kuweza hatimaye kutoka 7 hadi nambari 6.

Chapisha Maoni