Na Boniface Wambura, TFF
TIMU ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Tanzania, Ngongoro Heroes inarejea nchini leo (Aprili 7 mwaka huu) kutoka Kenya ambako jana (Aprili 6 mwaka huu) ilicheza mechi ya michuano ya Afrika.
Ngorongoro Heroes ambayo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 8.25 mchana kwa ndege ya Kenya Airways ilitoka suluhu na wenye Kenya katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Kanyetta uliopo mji wa Machakos.

Timu hizo zitarudiana jijini Dar es Salaam wiki tatu baadaye ambapo itakayofuzu itacheza raundi ya pili dhidi ya Afrika Kusini. Fainali za Afrika kwa vijana chini ya miaka 20 zitachezwa mwakani nchini Senegal.
Katika mechi nyingine za kwanza za hatua hiyo, Jumamosi Msumbiji iliifunga 2-1 Namibia, Malawi 1-1 na Bostwana, Swaziland ikafungwa 3-0 nyumbani na Lesotho, Shelisheli ikafungwa 2-0 nyumbani na Ethiopia, Djibouti 1-1 na Burundi, Sierra Leone ikaifunga 1-0 Guinea na Niger ikailaza 2-0 Kongo, Tunisia ikaichapa 3-0 Mauritania, wakati jana Liberia ilifungwa 1-0 na Gambia nyumbani na Chad ikaibwaga 1-0 Libya.
Chapisha Maoni