ALI YUSUPH SULEMAN TIGANA ALIKUWA MCHEZAJI NYOTA HAPA NCHINI
ILIPOISHIA JANA…….:-
“hiyo ni 9 kakini 10 wakati
tuliposhuka uwanja wa ndege jiji Dar es lalam hapo tulinyong’onyea kabisa kwa
kuwa tulipokea Taarifa ya kwamba mchezaji wa Mahili wa Soka Ramadhani Lemi
alikuwa amefariki dunia’anavuta pumzi na machozi yakamtoka kutokana na
kukumbuka jinsi ilivyokuwa’kisha anaendelea kusimulia; kiukweli majonzi
ambayo tulikuwa nayo ni makubwa sana basi moja kwa moja tukaenda kwenye mazishi
ya mchezaji mwenzetu,mungu awaweke mahali pema peponi wale wote ambao
walipoteza maisha siku ile.
SONGA NAYO..........................
Nilikimbia na laki moja ya Dewji.
“wakati nipo Pan Afrika kuna kipindi
tulicheza mechi ya kirafiki na wekundu wa msimbazi Simba,mchezo ambao nilicheza
kwa kiwango cha hali ya juu sana hali ambayo ilipelekea viongozi wengi wa simba
kunimezea mate ambapo baada ya mchezo ule, aliekuwa mdhanini wa simba Azim
Dewji aliwatuma watu wake kunitafuta ambapo walikuja hadi nyumbani na wakanichukua
na kunipeka ofisini kwake.
“siku ya kwanza kuingia ofisini kwa
Dewji niliogopa sana kwa kuwa sikuwai fikilia kama kuna siku nitafanikiwa
kuingia ofisini kwake kwa kuwa Dewji alikuwa Tajiri mkubwa,baada ya kuingia
ofisini kwake alinipokea vizuri na akaniambia kuwa ameridhika na uwezo wangu wa
uwanjani na alinitaka kusaini Simba,nilijifikiria sana kabla ya kumjibu kwa
kuwa Pan Afrika walikuwa wamenifadhili mambo mengi sana hivyo nilifikiria juu
ya kusaini simba bila kuwalipa fadhira zao,kwa woga nilimkubalia dili la
kusaini Simba.
“basi Dewji akanipa kitita cha
shiringi laki moja pia akiniambia kuwa anasafari ya kwenda uingereza
hivyo akirudi tutakamilisha kila kitu,kiukweli moyoni nilikuwa njia panda
na uamzi ambao nilipanga kuuchukua baada ya kufikiria kwa kina ni kuchezea Pan
Africa kwa kuwa tayari nilikuwa na mkataba nao.
“Dewji baada ya kutoka Uingereza
alinitafuta sana ili kusaini mkataba Simba kwa kipindi hicho aliwatuma watu
wake lakini nilikuwa nikiwapiga chenga kwa kuwa kipindi kile mawasiliano
yalikuwa magumu nilifanikiwa kuwatoroka adi msimu uliponza nikavaa uzi wa Pan
Afrika.
Itaendelea kesho tarehe
24-04-2014 atasimulia kuhusu imani za kishirikina uwanjani na zaidi kuhusu tukio
la kulewa pombe nchini Zimbabwe.
Itaendelea……………..
Chapisha Maoni