TIMU ya Taifa ya Tanzania taifa stars jumamosi wiki hii inatarija kuvaana na timu ya taifa ya Burundi Intamba Mu Rugamba ambayo inatarajiwa kuwasili nchini kesho (Aprili 24 mwaka huu) saa 12 jioni kwa ndege ya Kenya Airways ambapo mtanange huu utafainyika katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
vijana wa timu ya Taifa ya Burundi (Intamba Mu Rugamba)
Intamba Mu Rugamba itakuwa na msafara wa watu 28 wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi, na itafikia hoteli ya Accomondia. Mechi hiyo itachezwa kuanzia saa 10 jioni.
Tayari Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ipo kambini kwenye hoteli ya Kunduchi Beach ikijiandaa kwa mechi hiyo itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Kenya huku wakiwasubiri kwa hamu Intamba Mu Rugamba ambao ni moja kati ya vikosi bora afrika mashariki na kati ambapo kwa kipindi hiki taifa stars wana morali kubwa ya ushindi na kufanya vizuri katika michuano mbali mbali baada ya hivi karibuni uongozi wa timu hiyo kukiongezea nguvu kikosi hicho kwa kuwachukua vijana ambao waling'amuliwa hivi karibuni toka mikoa yote hapa nchini.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani. Kwa VIP A kiingilio kitakuwa sh. 20,000 wakati VIP B na C ni sh. 10,000. Mechi hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Na Boniface Wambura,Tff
Chapisha Maoni