SHAIBU KAMBANGA MCHEZAJI WA ZAMANI WA MAJI MAJI YA SONGEA,MAKALA
“Mwaka 1994 nilimshushia mwamzi kipigo ambaye
alikuwa akichezesha mechi yetu na Shinyanga Shooting kwa kosa la kuzidisha muda
wakati Dakika 90 na zile za nyongeza zilikuwa zimekamilika yeye kwa vile
hakutaka Maji Maji tushinde mchezo ule, na sisi tayari tulikuwa tunaongoza bao
1-0 aliongeza dakika nyingine takribani 7 hadi wapinzani wetu walipopata bao la
kusawazisha na akamaliza mpira.
Wakati mpira unaendelea nikamfuata mwamzi na kumwambia kama Shinyanga watasawazisha bao letu nitakupiga,kwa kweli mara baada ya mwamzi kumaliza mpira na matokeo kusomeka 1-1 kama ambavyo niliaidi sikufanya ajizi nilimfuata mwamzi na kumshushia kichapo cha maana ambapo wachezaji wenzangu walishitukia mwamzi yupo chini baadae polisi walinichukua na kunipeleka kituoni kwa kosa la kushika sheria mkononi.
lakini niliachiwa saa sita usiku na nikawa huru pia usiku ule ule nilikutana na yule mwamzi mara baada ya kumwona nikamwomba msamaha na baadae tofauti zetu zikawa zimeisha na tukaagana kwa amani,lakini kikubwa kilichomfanya awapendelee wale jamaa ni kwamba msimu ule Shinyanga walikuwa katika msitari wa kushuka daraja na walihaidi timu yeyote itakayokatiza ukanda wa ziwa kwa hali yeyote lazima itafungwa, mwamzi aliongwa lakini mchezo ulikuwa ni mgumu sana upande wao kutokana na ubora wa Maji Maji.
Baadae Fat walinifungia miezi 6 adhabu ambayo nililidhia kuitumikia,ila
kitu ambacho sikukipenda Fat hawakutangaza mapema kama nimefungiwa
walisubiri hadi Mchezo uliofuata kati yetu na Yanga Mjini Songea ndipo
walipotanpgaza nimefungiwa tayari nikiwa nimevaa jenzi sikuwa na jinsi nikavua
jenzi na kumpisha mwezangu”
Anasimulia Shaibu Kambanga ambaye alikuwa Mlinda Mlango wa Kutumainiwa wa Maji Maji ya Songea Mwaka 1989 hadi 2000,na kufanikiwa kuandika rekodi kubwa katika medani ya soka hapa nchini.
Kambanga ambaye ni mtoto wa kwanza katika familia yenye watoto 8 ya mzee Kamba,alizaliwa mkoani Mtwara eneo la Ligula na kupata elimu ya msingi katika Shule ya Ligula nyota yake ilianza kuangaza tangu akiwa shuleni hapo na kusifiwa na kila aliyemwona.
Katika maojiano maalumu na Jelamba viwanja anafafanua zaidi kuhusu maisha yake ya mpira;-
“Nilianza kucheza Soka la ushindani nikiwa na Toto Afrika ya Mtwara mwaka 19884 timu ambayo niliichezea kwa miaka 3 ambapo mwaka 1997 nikajiunga na Opec Fc ya masasi timu ambayo nilipata ujuzi wa kutosha kwa kuwa nilikutana na makocha kama Namanje pamoja na Molisi ambao walinifua vilivyo na nikacheza vizuri hadi timu yetu ikapata nafsi ya kushiriki ligi ya Mkoa kanda,tukiwa kanda Maji Maji wakalizika na mchango wangu wakanichukua moja kwa moja.
''Niliichezea Maji Maji toka mwaka 89 kwa mafanikio makubwa sana ambapo kufikia 2000 nikaamua kulipa kisogo soka na kuangaikia maisha yangu.
Simba yanga walishindwa masharti yangu.
''Wakati nacheza Maji Maji pia nilikuwa mwajiliwa kama dereva katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Ruvuma niliwaambia kama wanaitaji uduma yangu kwa dhati waniamishie kikazi katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salam kama dereva wa pale wote walishindwa na nikaendelea kuchezea Maji Maji.
''Sikutaka kwenda kucheza mpira Simba na Yanga bila kazi kwa kuwa viongozi wa timu hizo ni wanafiki sana mara nyingi wanawatelekeza wachezaji katika mazingira ya kutatanisha na wanaondoka mikono mitupu Mfano Omri Husein na John Alex waliachwa na timu hizo na waliathirika sana kisaikorojia.
Itaendelea kesho
tarehe 20-04-2014 ambapo atasimulia jinsi maji maji walivyopoteza pambano kwa
tatizo la ulevi,,,,,,,,,,,,
Usikose.
Chapisha Maoni