TAREHE 3-4-20104
JUMATATU ALIISHIA AKIWA NA MAJI MAJI MWAKA2006 SONGA NAYO ILI KUFAHAMU MENGI
Mwaka 2007 alipata
uhamisho kikazi kwenda mbinga hapo ndipo
ukawa mwisho wa kuitumika maji maji lakini alijiunga na Mbinga United timu ambayo ameichezea hadi mwaka jana 2012 ambapo
kwa sasa amestaafu kucheza soka la ushindani,na anachezea timu za
veteran,anasimulia Hamis Mtepa Kisha anaendelea;-
Nilizuiwa kuvaa jezi
ya Bandari Mtwara.
“wakati Tanesco waliponiamishia Mtwara kikazi timu ya
baadari walilidhika na uwezo wangu na
walitoa donge nono kunisajili lakini Tanesco walinizuia na kauli ilikuwa ni ile
ile kwamba asietaka kufanya kazi Tanesco akacheze mpira, sikuwa na jinsi niliishia kufanya nao mazoezi pekee
ingawa kwa kipindi kile ilikuwa bahati kubwa sana kuchezea timu ambayo ilikuwa
na jina kubwa kama Bandari ya Mtwara,na atimayenikaishia kuchezea timu za
mtaani.
Mechi Kali.
“siwezi kusahau mechi
kati ya Tanesco dhidi ya Yanga uwanja wa Maji Maji mjini Songea ,kwangu mimi ulikuwa ni mchezo
wa kwanza kusimama langoni dhini ya Timu kubwa na ukizangatia kwa upande wa
Yanga ilikuwa mechi yao ya kwanza mara baada ya kuchukua ubingwa wa Afrika
Mashariki na Kati nchini Uganda mchezo ulikuwa mgumu sana kwa kuwa tulikutana na wachezaji
wenye majina makubwa kiasi kwamba
tulikuwa tukiyasikia Radioni pekee.
“tulijitaidi sana kipindi cha kwanza tuliwashindilia yanga
bao moja kwa nunge lakini kipingi cha pili mambo yakabagilika kama waswahili
wasemavyo mtoto mdogo alali na pesa
Yanga walitukimbiza sana ambapo walifanikiwa kupata mabao mbili yaliyowekwa
kimiani na Mahamed Husein Maarufu kama mmachinga hadi mwisho wa mchezo yanga
waliibuka na ushindi wa bao 2-0.
Ushirikina
“Mambo hayo kwenye mpira yapo lakini kwa kiasi kikubwa uchangia kushuka kwa
ufanisi katika timu kwa kuwa viongozi wa timu badala ya kuwalipa wachezaji vinzuri wanajiziuka na imani za kishirikina,kuna
kipindi Maji Maji walimsajili mchezaji Idifonzi Hamlima toka Mtwara mchezaji ambaye alikuwa tishio
kwa soka la hapa mchini baada ya kutua Maji Maji akacheza chini ya kiwango kwa
makusidi na akasema awezi kutumia nguvu nyingi wakati ujira mdogo.
SIKU 100 za Malinzi amesahau
kusini.
“Moja ya maeneo ambayo yana vipaji halisi vya mpira uwezi
kusahau mkoa wa Ruvuma na nyanda za juu kwa ujumla, lakini katika siku Mia za
utawala wa Rais mpya wa Shirikisho la Soka hapa nchini ajakakanyaga Ruvuma hii
inaashiria kuwa mchango wa mkoa wa Ruvuma wa kutoa wachezaji wenye vipaji vya
soka hapa nchini kwa sasa hautambuliki ndio maana mtu wa mwisho kuchezea taifa
Stars kwa Mafanikio Toka Ruvuma ni Stivin Mapunda Garincha,
“Lakini ndani ya siku hizo 100 tayari malizi ameshaenda
mikoa ya kasikazini hivyo namshauri Rais wa wa soka ili kuendeleza soka la hapa
nchini kwa vitendo lazima afanye ziara kanda zote na kuchukua maoni ya wadau wa
soka na kufanyia kazi.
Nilipenda kuchezea
Simba sikupata nafsi.
“mimi naipenda Simba toka nikiwa mdogo kiasi kwamba nilijitaidi kucheza kwa bidii ili samba
wanichukue lakini mambo yakawa kinyumbe kabisa sikupata ofa yeyote ya
kusajiliwa na samba,hata kuwasikia watu mtahani nataka kusajiliwa na samba
sikusikia kabisa,lakini adi leo mimi ni Simba damu.
Soka la zamani na
sasa.
“zamani tulikuwa tukicheza kwa moyo wote,ilikuwa faraja sana
kwa mchezaji kuingia uwanjani ukiwa umevaa jenzi huku ukitumia timu yako kwa
dhati bila kujali malipo,lakini wachezaji wa siku hizi ingawa awafanani na pesa
wanayochukua ni wavivu sana tukilinganisha na zamani.
Nilitema mpira nikafungwa.
“kila nikikumbua huwa naumia sana,ilikuwa kati ya Tanesco na
Yanga uwanja wa Maji Maji Songea ilikuwa baada ya yanga kusawazisha bao kipindi
cha kwanza tayari matokeo ubaoni yalisomeka bao 1-1,basi kuna mpira ulipigwa
toka winga ya kushoto mabeki wote wa Tanesco waliuzwa mpira ukanaswa na
mshambuliaji wa yanga akaachia shuti kali! Mimi nikatema mpira basi wakati
naukimbilia kwa mara nyingine wote wawili tukaanguka chini laini mchezaji wa
yanga akaniwai na akadokoa mpira kwa mguu ubao ukasomeka yanga 2,sisi 1 hadi
mwisho wa mchezo.
Mchazaji Mkali.
“Ramadhani Singano “messi” ananikosha sana ni wachezaji
wachache wenye uwezo wa kuingia na mpira eneo 18 bila woga, wachezaji
wengi mara nyingi ni waoga kuingia eneo
hilo badala yake hurudisha mpira nyuma.
Ushauri Taifa Stars &Mbinga
“umakini uwepo katika soka la nchi yetu la sivyo! uwezekano
wa kushiriki kombe la dunia ni kuanzi miaka ya 2025 na kuendelea baada ya
kuangamia kizazi hiki,kushiriki fainali za kombi la dunia yanaitajika
maandalizi ya kweli.
“Baada ya miaka Kadhaa Wilaya ya mbinga itakuwa na timu ligi
kuu kwa kuwa uchumi wa Mbinga unaenda kasi sana na mara nyingi wadau wa soka
wanakaa vikao kuhusu jinsi ya kuendeleza soka
soka la mbinga,kuna timu kama mbinga united itafanya vizuri.
Maisha ya sasa.
“Mimi ni mfanyakazi wa Tanesco wilayani Mbinga,pia ni kocha
msaidizi wa Mbinga United,umri wangu ni miaka 42, kwa sasa sina mke nina watoto
watatu,anaitimisha Hamis Mtepa ambaye
anawakumbuku sana Iddi Panzi
[father],Stivin Nemes [maji Maji] pamoja na Amis Makana [Coastal] ambao walimpa
mwanga wa kucheza kwa kujituma.
Chapisha Maoni